Na Chrispino Mpinge
Wizara ya Afya , Maendeleo ya
Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha
maabara nne za Kanda ili kuboresha huduma za vipimo vya upimaji wa kifuu
na kifuaa kikuu sugu.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha na kusogeza huduma karibu za upimaji wa kifuaa kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu makadirio ya
mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17.
Amezitaja hospitali hiso ambazo
zitakuwa na maabara hizo kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali
ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali
ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.
Waziri Ummy aliongeza kuwa
Wizara hiyo itaendelea matibabu ya kifua kikuu sugu katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bugando.
Aidha ,Waziri huyo aliongeza
kuwa Wizara imefanikiwa kufikia idadi ya vituo 547 vinavyotoa huduma
shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI nchini .
Hatua hii inalenga kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wenye maambukizi mseto ya Kifuua Kikuu na UKIMWI kupata huduma sehemu moja.
Waziri Ummy aliongeza kuwa
chini ya utaratibu huo , Wizara imefanikiwa kutoa huduma watu 692,642
wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI (WAVIU) ili kubainisha
uwepo na kutokuwepo kwa maambukizi ya kifua kikuumiongoni mwao.
Alisema kuwa kati ya hao watu 26,218 waligundulika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu na walipatiwa matibabu.
Aidha , Waziri huyo alisema
kuwa katika mwaka ujao wa fedha ,Wizara hiyo itaendelea kutoa huduma za
matibabu ya kifua kikuu sugu kufikia hospitali kumi za mikoa ya Dar es
salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Tanga, Shinyanga, Geita
na Mara.
Alisema kuwa Wizara itaongeza
uwezo mikoa 16 yenye viwango vya chini kabisa vya uibuaji wagonjwa wa
kifua kikuu ili kuongeza kasi ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.
Katika mwaka ujao wa fedha
Wizara hiyo iliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya matumizi ya
Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ys shilingi
845,112,920,056.00.
No comments:
Post a Comment