Monday, 2 May 2016

ADC:Hamad Rashid ndo analeta Migogoro katika chama

Na Kalonga Kasati

 Katika Siasa Hakuna adui wa kudumu Wala Rafiki wa kudumu Hilo limeendelea katika vyama Vingi vya hapa nchini Vinaanzishwa kwa Malengo Mazuri ila Baadaye Waanzilishi wa Vyma Hivi Au wanachama Wanapoamua kumuondoa Mtu katika Nafasi Fulani ila kunapotokea Migogoro Wakilaumia na kumtafuta nani Mchawi Mchawi Wanae Wanashindwa kumuona

Mchezo wa Siasa ni Mzuri Sana pale Mnapokuwa Sawa kimtazamo lakini mnapotofautiana Mambo huwa ndivyo sivyo, imeshuhudiwa Migogoro Mingi kwenye Vyama vya Siasa nchini ikiwemo CUF na ACT Wazalendo moja ya vyama Vilivyowahi kuwa na mgogoro.

Lakini Mgogoro wa Chama cha Allience For Democratic Change (ADC) Umezidi kuchukua Sura mpya kila Uchwao Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Fransis Mutungi kuiomba Bodi ya Udhamini ya chama hicho kuurudisha Uongozi halali wa chama hicho ambao Waliusimamisha kwa muda, jambo ambalo limekuwa Gumu kwa Bodi hiyo kukubali kuachia Ngazi.

Hivyo Mwenyekiti wa Chama hicho aliyesimamishwa na Bodi ya Wadhamini Saidi Miraji Amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kusimamia Maamuzi yake na kukitaka Chama chake cha ADC kutoendeshwa na Maamuzi ya mtu Mmoja ambaye ni Mlezi wa chama hicho Hamad Rashid anayeonekana kuchochea mgogoro huo kwa Maslahi yake binafsi.

Huku akieleza Kuwa chanzo cha Mgogoro ndani ya Chama hicho ni Baada ya Yeye kumuonya Mlezi wa Chama hicho Hamad Rashidi kutumia Jina la Mwenyekiti kufanya Baadhi ya Maamuzi ikiwemo kutangaza kuwa ADC itashiriki ule Uchaguzi wa Marudio Visiwani Zanzibar katika kikao chake na Waandishi cha Desemba 29 Mwaka Jana, Bila kuwepo kikao Cha kuridhia hayo, hivyo anadaiwa kujichukulia Maamuzi yake Binafsi.

Aidha amemuomba Radhi Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Fransis Mutungi kutokana na Ofisi Yake kuhusishwa kumbeba Mwenyekiti huyo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo Jambo ambalo sio la kweli, halikadhalika Baraza la Vyama vya Siasa kwa kuitwa Matapeli wa kisiasa na Katibu Mkuu huyo, huku akieleza kuwa katibu analitumia kivuli cha ADC kuharibu taswira yake.

No comments:

Post a Comment