Muungano wa
upinzani nchini Kenya CORD unafanya maandamano katika miji mikuu nchini Humo kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC)
kujiuzulu.
Viongozi wa muungano huo wamesema maafisa hao hawawezi kuandaa uchaguzi huru na wa Haki mwaka ujao.Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na marungu kutawanya maandamano sawa na Hayo Jumatatu wiki iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano hayo.
- Kwa Picha: Maandamano ya upinzani Nairobi
- Odinga: Tume ya uchaguzi ni sharti ibadilishwe

Maduka mengi yamefungwa kutokana na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo na kutokea kwa Uporaji.
No comments:
Post a Comment