Tuesday, 3 May 2016

Mose Iyobo:Mimi na Mama Cookie Tupo Vizuri na Hatuja Kwaruzana






Baada ya kuzagaa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa dansa wa Diamond, Mose Iyobo na mama mtoto wake Aunt Ezekiel, wameachana na kila mtu Anaishi kwake, Mose amefunguka na kusema mahusiano yao yapo salama kabisa.

Akizungumza Mose alisema Habari za kwamba Ameachana na Aunt Ezekieli kisa Aunt amechepuka sio za kweli.

“Hivi vitu naviona na najua ni vitu vya kuzusha tu, mimi na mama Cookie tupo Vizuri na hatuja kwaruzana. Kwa hiyo hivyo vitu sio vya kweli na wala Hatujaachana,” alisema Mose.

“Kugombana tunagombana, ni vitu vidogo vigogo vya ndani ya nyumba. Pia Nilisikia sisi tumeachana kila mtu anaishi kwake, sio kweli, kipindi hicho mimi Nilisafiri sasa walivyokuwa wanamuona yupo peke yake, ndio wakazusha Hivyo,” aliongeza.

Mose amesema hizi tetesi hazimuumizi kichwa kwa kuwa tayari anajua sio vitu Vya kweli

No comments:

Post a Comment