Saturday, 14 May 2016

Mjumbe wa Soka Wilaya ya Morogoro Alex Bulengwa amesimamishwa kwa tuhuma za ubdhirifu wa fedha kiasi cha 225,000




Dustan Kamala

Chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA) kimemsimamisha uanachama mjumbe wake, Alex Bulengwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kiasi cha 225,000 zikiwa ni mapato ya kiingilio (Get Collection) katika ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Manispaa daraja la nne msimu wa mwaka 2014/2015.

Mjumbe huyo anadaiwa kushindwa kuingiza benki katika akaunti ya chama hicho na kuisababishia hasara ya kiasi hicho.

Akizungumza  mjini hapa, Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka wilaya ya Morogoro, (MMFA) Kafale Maharagande alisema kuwa Mei 14 (leo) kunafanyika mkutano mkuu maalumu, ajenda kuu ni mbili ikiwemo ya kujadili marekebisho ya katiba na usimamishwaji wa uanachama wa mjumbe huyo.

Maharagande alisema kuwa mkutano huo unafanyika kwenye uwanja wa jamhuri kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana na tayari barua za mwaliko zimetumwa kwa wajumbe ambao ni viongozi wa vilabu vya soka vinavyoshiriki ligi ya chama cha soka Manispaa.

“Ajenda ni mbili moja ya ubadhirifu wa mali za chama fedha taslimu kiasi cha sh225,000 ambazo ni mapato ya kiingilio (Get Collection) na ajenda nyingine ni kujadili marekebisho ya katiba na maamuzi yatafanywa na wanachama wa mkutano mkuu maalumu Mei 14 (leo) uwanja wa jamhuri Morogoro”.alisema Maharagande.

Maharagande alisema kuwa kikao cha mkutano huo kilipangwa kufanyika Mei 15 (kesho) katika uwanja wa jamhuri lakini kutokana na muingiliano wa ratiba ya ligi kuu Tanzania bara kutakuwa na mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Simba SC siku hiyo wameamua kurudisha nyumba tarehe ya kufanyika kwa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment