Na. Chrispino Mpinge
ABIRIA
wa mabasi ya mwendo wa haraka wametakiwa kupanda bure mabasi hayo hadi
siku ya mwisho tarehe Jumapili Mei 15 mwaka huu kabla ya kuanza kutozwa
nauli
Akizungumza
katika kipindi Maalum cha “Malumbano ya Hoja” kilichorushwa jana (Mei
12, 2016) katika Kituo cha Televisheni cha ITV, Mkurugenzi wa Mfumo na
Uendeshaji wa Wakala wa Usafiri wa Haraka jijini Dar es salaam (DART)
Mhandisi John Shauri, Utaratibu huo umepangwa ili kuwawezesha watumiaji
wa mabasi hayo kupata elimu ya uelewa kuhusu taratibu za huduma ya
usafirishaji zinazotolewa na mabasi hayo.
Mhandisi
Shauri aliwataka abiria wanaotumia mabasi hayo yanayofanya safari zake
Kivukoni – Kimara, Kivukoni – Morocco, Kariakoo – Kimara na Kariakoo –
Morocco kuitumia vyema fursa ya elimu ya uelewa itakayotolewa na
wafanyakazi wa mradi huo walipo katika vituo vya mabasi.
Aliongeza
mfumo wa usafirishaji wa mabasi umezingatia pia mahitaji ya watu wa
makundi maalum wakiwemo walemavu, ambapo mwanzo na mwisho wa vituo hivyo
kuna mageti maalum sambamba kutenga viti maalum ndani ya mabasi hayo
vitavyotumiwa na watu wenye ulemavu.
Kwa
upande wake Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya
Kinondoni SSP Awadhi alisema pamoja na kuwepo mradi huo sheria za
barabani zinapaswa kufuatwa na waendeshaji wa mradi huo pamoja na
wananchi kwa ujumla, vilevile ili wote kwa pamoja wakaelewa matumizi ya
mabasi hayo na kufata utaratibu uliowekwa.
Naye
Meneja Uhusiano wa UDA, Bwana Dennis Mgaya aliwataka abiria wapande
mabasi hayo kwa kutumia vituo vilivyopo kwa dhamira ya kujifunza, badala
ya kutumia muda mwingi kuzunguka ndani ya mabasi hayo.
Jumla
ya mabasi yaendayo haraka 138 yamewasilia nchini kwa ajili kutoa
huduma ya usafirishaji kwa jiji la Dar es salaam ili kupunguza
msongamano kwa wakazi wa jiji hilo, na tayari mabasi hayo yameanza kutoa
huduma tangu mwanzo wiki.
No comments:
Post a Comment