Polisi wilayani Arumeru j iliwashikiliwa kwa muda mbunge wa
Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na madiwani 35 wa Chadema kwa tuhuma
za kuvamia eneo na kuharibu mali.
Viongozi hao, wiki iliyopita
walivunja uzio wa mabati uliojengwa jirani na halmashauri na
mfanyabiashara Itandumi Makere, wakimtuhumu kupata eneo hilo la Serikali
kinyume cha sheria.
Nassari na madiwani hao, walishikiliwa kwa
muda baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Usa River. Viongozi
hao, baada ya kufika polisi saa tatu asubuhi walihojiwa kwa zaidi ya saa
sita kwa tuhuma hizo.
Nassari alisema kitendo hicho cha kufikishwa polisi na kuhojiwa hakiwatishi kwani wanachokifanya ni kutetea ardhi ya Wameru.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Meru, Wille Njau alisema wamedhalilishwa na hatua
hiyo kwani walikuwa wanatekeleza uamuzi ya Baraza la Madiwani.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kuhojiwa kwa mbunge na
madiwani hao na kusema wanafanya uchunguzi na jalada litawasilishwa kwa
mwanasheria mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment