Wednesday, 11 May 2016

Mbeya Yanga walituzidi Ujanja

 

 Na Yahya Njenge

Kocha mkuu wa timu ya Mbeya City Kinnah Phiri ametaja sababu iliyopelekea kikosi chake kupoteza mchezo wao dhidi ya Young Africans kwenye uwanja wao wa nyumbani (Sokoine) kwa kipigo cha magoli 2-0.

Mmalawi huyo alisema uzoefu wa wachezaji wa Young Africans ndio sababu kubwa iliyowapa Ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa jana huku akisema kukosa uzoefu kwa washambuliaji Wake kumewafanya washindwe kupata bao kwenye mechi ya leo.

Phiri ambaye alijiunga na Mbeya City kuchukua mikoba ya mzalendo Meja Mstaafu Abdul Mingange alisema, timu yake ilicheza vizuri lakini kitu kilichowafanya wapoteze mchezo wao ni uzoefu wa wachezaji wa Young Africans na si vinginevyo
 
“Tulikosa umakini kwenye safu yetu ya ushambuliaji lakini tumecheza vizuri nja kutengeneza Nafasi nyingi za kufunga ambazo tumeshindwa kutendea haki”, alisema Phiri

“Kama ulivyoona, tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tulishindwa kufunga. Wapinzani wetu wametufunga kutokana na uzoefu wao hakuna kingine” aliongeza kocha huyo kutoka Malawi

City waliruhusu goli la kwanza dakika ya 16 likifungwa na beki kutoka nchini Togo, Vicent Bosou ambaye aliruka bila kukabwa na kuukwamisha mpira wavuni.

Uzoefu wa mlinda mlango wa Mbeya City Juma Kaseja uliwasaidia Mbeya City kutokana na kufanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya washambuliaji wa Young Africans ambao waliliandama goli la City kila mara.

Mrundi Amis Tambwe akaifungia Young Africans bao la pili kwa mkwaju mkali ambao aliuachia akiwa nje ya box na kumuacha Kaseja asijue la kufanya kutokana na kitendo chake cha kuwa mbele kidogo ya lango.

No comments:

Post a Comment