Na Mwamvita Mtanda
Kikosi
cha Mbeya City Fc tayari kimetua mkoani Shinyanga tayari kwa mchezo wa
duru ya lala salama ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya
wenyeji Mwadui Fc, mchezo Uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye
uwanja wa Mwadui uliopo nje kidogo ya mji huu wa kanda ya ziwa.
Afisa habari na mawasiliano wa
kikosi cha City, Dismas Ten amesema leo asubuhi kuwa nyota wote 18
waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wako kwenye hali nzuri kiafya na
kinachosubiriwa ni dakika 90 za siku ya mchezo.
“Tumekuja hapa na wachezaji
18,wote wako kwenye hali nzuri kwa mujibu wa daktari wetu, asubuhi hii
tumefanya mazoezi mepesi na sasa tunasubiri siku ya mchezo,tunafahamu Wapinzani wetu wana timu nzuri na pia wanacheza nyumbani, hilo halitupi
shaka sana kwa sababu tuna kikosi ambacho kinaweza kushind popote,
tumejiandaa vizuri na hilo ndiyo lengo letu”, alisema.
Kuhusu wachezaji waliosafiri
kutoka jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo huo Ten alisema kuwa City
imelazimika kumuondoa kikosini mlinzi Hassan Mwasapili kutokana na kuwa
na kadi tatu za njano hivyo hawezi kuwa sehemu ya mchezo huo.
“Tumemuacha Mwasapili hii ni kwa
sababu ana kadi tatu za njano,kwa vyovyote tusingeweza kumtumia, badala
yake tumesafiri na Yusuph Abdalah mbaye amekuwa kwenye kiwango kizuri
mazoezini hasa baada ya kupona majeraha” alisema Ten, huku akiwataja
nyota wengine walio kwenye msafara huo kuwa ni pamoja na –
Juma Kaseja, Hanningtony
Kalyesubula, John Kabanda,John Jerome,Yusuph Abdalah,Yohana Moriss,Tumba
Sued,Haruna Shamte,Kenny Ally,Ramadhan Chombo,Raphael Daud, Geoffrey
Mlawa,Salvatory Nkulula,Joseph Mahundi na wengine.
No comments:
Post a Comment