Madee nimetumia vazi la kanzu kama mavazi mengine
Na Tabu Mullah
Vazi la Kanzu huvaliwa mara nyingi na
waumini wa Dini ya Kiislamu ikiwa ni kielezo cha dini yao, japo kwa
mujibu wa dini hiyo Mchamungu ndio mtu mwema kwa Mungu haijalishi amevaa
kanzu au lah cha muhimu afuate yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa
na Mwenyezi Mungu.
Kwenye Tasnia ya Muziki tumeona baadhi
ya wasanii mbalimbali wakitumia vazi la kanzu kwenye video zao akiwemo
Davido ambaye alivaa vazi la kanzu kwenye wimbo wake wa The Sound huku
Niki wa Pili wa Kundi la Weusi nae akivalia vazi hilo kwenye video ya
Bum Kum Bum, naye msanii Madee ametumia vazi hilo katika video yake ya
wimbo ya Migulu Pande anayotarajia kuiachia siku ya Jumatatu.
Picha
aliyopost Madee kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa amevalia vazi
hilo la kanzu imezua utata kwa baadhi ya watu kudai kuwa ameidhalilisha
Dini ya Kiislamu na mmoja wa mameneja wa msanii huyo maarufu kama Dj Kman
au Ally Taletale ambaye amefunguka kuwa wametumia vazi la kanzu kama
mavazi mengine.
Ndio maana katika video hiyo
waliyoiachia wamechanganya mavazi mbalimbali, hivyo hawajaudhalilisha
uislamu, na kuongeza kuwa kuna baadhi ya nchi kama Dubai watu huvaa vazi
hilo na kwenda sehemu ambazo sio za ibada ikiwemo kumbi za kuonesha
mpira
No comments:
Post a Comment