
Mabaki ya ndege na
vipande vya wanadamu vimepatikana vikielea kwenye Bahari ya
Mediterranean na makundi yanayotafuta ndege ya kampuni ya EgyptAir
iliyotoweka Alhamisi.
Waligundua pia viti na mizigo ya abiria.Katika muda wa maaa machache yaliyoipita takwimu zinaonyesha kuwa vingora vya kuashiria kwamba moshi upo, vilianza kulia kabla ya ndege hiyo kutoweka ikiwa na abiria 66.

Mjini Cairo ambapo ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Paris, Ufaransa ilikuwa ikitarajiwa, jamaa Na marafiki ya abiria wamefanya ibada maalum katika misikiti.
No comments:
Post a Comment