Kesi ya kupinga Ubunge wa Kinondoni umeahirishwa mpaka Mei 19 ya Mwezi huu
Na Chrispino Mpinge
Baada ya Kesi namba 3/2015 ya kupinga Matokeo ya Uchaguzi ya Mbunge wa
Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam Maulidi Mtulia (CUF)
iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Iddi Azan (CCM)
kuahirishwa kusikilizwa mara 3 mfululizo ndani ya wiki hii kwa sababu
mbalimbali, Jaji Chocha kutoka Mahakama ya Mbeya ameahirisha tena
kusikilizwa kwa shauri la kesi hiyo leo na kuipangia Mei 19 ya mwezi
huu.
Madai ya msingi yamebaki manne kutoka
nane, hivyo hatua ya kuahirishwa kwa kesi hiyo imefuata baada ya
Abubakari Salim Wakili wa upande wa Iddy Azzan kuiomba mahakama impe
muda wa wiki moja wa kuandaa mashahidi 10 na fomu za viapo, ambapo Jaji
Choche alikubali.
Abubakari Salim
Upande wa Mshitakiwa namba moja (Maulidi
Mtulia Mb) umethibitisha kuwa na wenyewe watapeleka mashahidi 10,
wakati upande wa mshitakiwa namba 2 na 3 (Mwanasheria Mkuu na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi), na wao watapeleka mashahidi 15.
Maulidi Mtulia (Aliyavalia suti ya Bluu) akizungumza na wananchi
wake wa Jimbo la Kinondoni waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Madai ya Msingi manne yaliyobakia katika kesi hiyo
No comments:
Post a Comment