Ajenti mmoja wa
zamani wa shirika la ujasusi la marekani CIA, amekiri kuwa ndiye Aliwafahamisha polisi wa Afrika kusini aliko rais wa zamani wa nchi hiyo
Nelson Mandela,
Ambaye baadaye alikamatwa na kufungwa miaka 27 jela kwa
kupinga utawala wa wazungu.
Ufichuzi huo uliofanywa na gazeti la
Sunday Times muda mfupi kabla ya ya kifo cha jasusi Mmarekani Donald
Rickard, unafichua kuwa Mandela ambaye alikuja kuwa rais wa kwanza Mweusi nchini Afrika kusini alikuwa akifuatiliwa na CIA.Mandela alikamatwa mwaka 1962 saa za usiku karibu na mji wa Durban akijifanya kuwa Dereva wa texi, wakati gari lake lilisimamishwa kwenye kizuizi cha polisi.
Sasa ufichuzi wa ajenti huyo wa zamani wa CIA marehemu Donald Rickard unathibitisha Ramsi kuwa ni yeye aliwajulisha polisi hatua ambayo ilisababisha Mandela kuwa mfungwa Maarufu zaidi duniani.
Wakati huo kiongozi yeyote wa kundi lililojihami alitajwa kuwa gaidi na mkomisti hatari zaidi Nje ya muungano wa usovieti na tisho kwa nchi za magharibi.
Hata hivyo Mandela alikana kuwa mwanachama wa chama cha kikomisti.
Ufichuzi huo unatarajwa kuiwekea shinikizo CIA kuitaka kutoa habari kuhusu kuhusika kwake katika kukamatwa kwa Nelson Mandela na uungaji mkono wake serikali ya ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment