Je Vyombo Vya Habari ni Kweli ni Muhimili wa Nne wa Dola?
Na Kalonga Kasati
Leo ikiwa ni siku ya Uhuru wa Habari kwa Hapa Tanzania Tumezidi kurudi Nyuma kuminya Vyombo vya Habari kutoonyesha Bunge live kwa Maslahi ya Watu Wachache tu huku Tukiwakandamiza Raia kupata Haki yao ya Msingi kupata Habari
Badala kuenda Mbele na kasi ya Dunia inavyokwenda sisi Tukirudi Nyuma Wakati Tulikuwa Tunapigania Habari za Mahakama kuonyesha live Sasa Tumerudi Nyuma huku bunge Halitakiwi kuonyesha live je Freedom of Press iko wapi?au tunajivurusha kusema Tuna Uhuru Wa vyombo Vya habari hapa Tanzania
Wanahabari Wengi Wamepoteza Maisha yao kutokana na kupigwa na wengine kupoteza Maisha wakiwa kazini kwa ajili ya kuhabarisha umma mfano wa waandishi waliopoteza Maisha Daudi Mwangosi aliyeuwa kinyama na polisi Saed Kubenea aliyemwagiwa tindikali Machoni Mhariri a New Habari Absalom Kibanda aliyetolewa kucha hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari Waliopatwa na matatizo
Wanasema Vyombo vya Habari ni Muhimili wa nne wa Dola kwa Mdomo kimatendo Haviendani kabisa ni kijikosha Mbele za Jumuiya za kimataifa
Mei 3 kila Mwaka Wanahabari hapa nchini Huungana na Wanahabari Wenzao Duniani kote katika Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujadiliana Mambo Yanayoihusu Tasnia hiyo
ambapo leo hii Wamepaza Sauti zao kwa Serikali kupitia kwa Waziri Mwenye Dhamana kukutana na Wamiliki wa Vyombo vya Habari lengo likiwa ni
kujadili na kutatua changamoto Zinazozikumba Tasnia hiyo.
Akizungumza Mtangazaji
wa Kituo cha EFM Redio Emmanuel Kapanga alisema Uhuru wa Vyombo vya Habari hapa nchini Bado Haukidhi Viwango kutokana na Waandishi wa Habari
kutopewa kipaumbele huku Changamoto ya kutopewa Mikataba na Waajiri wao
ikiendelea kuwatesa na kupelekea Kugombea Bahasha Jambo ambalo ni
kinyume na Maadili ya Tasnia Hiyo.
Naye Tunu Hassan Mtangazaji wa Michezo EFM Redio amesema Bado Waandishi Wanaa Nyanyasika na kubaguliwa na
Maafisa Habari pindi Wanapokwenda kuchukua Habari na Huchangia kwa kiasi
kikubwa kuiuwa stori kwa kuficha Baadhi ya Vitu Vingine.
“Sisi Waandishi wa Habari hatupendani hao Maafisa Habari Wanasahau walipotoka, Utakuta Unaenda katika stori Wanabagua Vyombo vya kuhudhuria katika
kikao chao hiyo inakuwa Haipendezi”. Amesema Tunu
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari hapa nchini amefanyika Mei 3katika Hoteli ya Malaika
Beach Resort Jijini Mwanza, huku waathirika wa Ukiukwaji wa Uhuru wa Habari wakitoa Ushuhuda Juu ya changamoto walizokabiliana nazo Wakati wa Utekelezaji wa Majukumu yao.
No comments:
Post a Comment