Wednesday, 18 May 2016
Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 26
Na Mwamvita Mtanda
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Boniface Mkwasa ametaja kikosi chenye majina ya wachezaji 26 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya pamoja na ile ya kufuzu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri.
Katika kikosi hicho nahodha wa zamani, Nadir Haroub amerudishwa kundini licha ya awali kutangaza kujiuzulu kuchezea timu ya taifa.
Haroub ameitwa kuziba pengo la Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za Njano na hivyo kuikosa mechi ya Misri Juni 4.
Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini tarehe 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya utakaochezwa tarehe 29 Mei jijini Nairobi.
Baada ya hapo Taifa Stars itarejea Dar kukamilisha maandalizi ya kuivaa Misri katika mchezo ambao inahitaji ushindi wa angalau mabao matatu kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwakani.
Kikosi kamili: Kikosi cha Stars:
Walinda Milango: Deo Munish ( Yanga), Aishi Manula (Azam) Benno Kakolanya ( Prisons).
Walinzi: Juma Abdul, Haji Mwinyi,Nadir Haroub (Yanga ), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris ( Azam), Mohamed Tshabalala (Simba), Andrew Vicent ( Mtibwa Sugar).
Viungo: Himid Mao, Farid Mussa ( Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya ( Mtibwa Sugar ),Hassan Kabunda ( Mwadui ), Juma Mahadhi (Coastal Union). Ismail Issa Juma ( JKU)
Washambuliaji: Elias Maguri ( Stand United), John Bocco ( Azam) Ibrahim Hajib ( Simba), Mbwana Samatta ( Genk GRC, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu ( TP Mazembe)
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment