Pyongyaung. Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku
mikusanyiko inayoashiria kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama vile
inayohusu unywaji na uimbaji.
Ametaka wananchi kutosherehekea sikukuu hiyo na wanaopenda kufanya
hivyo, waitumie Desemba 24 kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake
aliyezaliwa siku kama hiyo mwaka 1919.
Kiongozi huyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha
vinadhibiti mikusanyiko yote ambayo inaendana na maadhimisho ya
Krismasi.
“Ni marufuku watu kukusanyika na kufanya mambo kama ya unywaji au kuimba
katika sikukuu ya Krismasi,” chanzo kimoja cha habari kimenukuu taarifa
ya kiongozi huyo.
Kim Jong Un amekuwa akichukua hatua kuzua kuenea kwa utamaduni kwa
kigeni na amedhibiti vyombo vya habari kutotangaza taarifa zozote
zinazoienzi sikukuu hiyo kama hatua ya kupiga marufuku Krismasi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa watu ambao
wanasema vyuma vimekaza na wale ambao wamekuwa wakisambaza takwimu
mbalimbali za kupikwa kukamatwa na kuwekwa ndani na baadaye kupelekwa
mahakamani.
Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo
la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na
masuala ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma
vimekaza ili hala watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.
"Ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana
ndiyo maana kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi
tuwasikilize watu wa takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu
tofauti na zile walizonazo watu wa takwimu. Mtu anasema vyuma vimekaza
wakati watu wa takwimu wanasema vyuma vimefunguka watu hawa wanatakiwa
kukamatwa na kuwekwa ndani ili wakajifunze kutoa takwimu huko" alisema
Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameagiza watu ambao watatoa taarifa zozote
ambazo zipo kinyume na takwimu walizonazo watu wa takwimu wafikishwe
mahakamani "Mimi ningekuwa hakimu watu wa namna hiyo wangepewa adhabu
zote mbili kulipa faini na kufungwa"

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono.
Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na
amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).
Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis amesema leo Jumatano Desemba
20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 2:45 usiku wakati akiondoka
hotelini kurejea nyumbani.
Hamis amesema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.
“Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaiwa Ansbert Sweetbert
ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” amesema.
Amesema, “Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye
aliyempeleka KCMC na alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na
madaktari KCMC walimpa msaada mkubwa.”
Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alipotafutwa leo mchana
amesema bado maumivu aliyonayo ni makali kutokana na kuvunjika mkono.
“Bado nina maumivu makali. Nashukuru sana Mungu na jopo la madaktari limeshakutana na watafanya uamuzi,” amesema.
Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano
Ronaldo anatarajia kujenga hospitali ya watoto jijini Santiago nchini
Chile.
Hospitali hiyo ambayo itajengwa na Ronaldo akishirikiana na
mfanyabiashara kutoka nchini Italia Alessandro Proto, inatarajiwa
kukamilika kabla ya mwaka 2020.
Jiji la Santiago umekuwa mji wa kwanza kati ya mingine ambayo Ronaldo na
Proto wanampango wa kujenga hospitali hizo za watoto barani Amerika
Kusini.
Ronaldo amekuwa mdau mkubwa wa kuchangia damu kwaajili ya watoto wenye
matatizo mbalimbali ambapo amefanya hivyo mara kwa mara. Pia nyota huyo
ni balozi wa “Save the Children, Unicef “ na “World Vision”.

Msimu wa sikukuu za Xmass umefika, na kama kawaida kwa wenzetu barani
Ulaya huwa katika kipindi hichi ndio kipindi ambacho timu zinakuwa na
mechi nyingi sana, leo tuone jinsi timu kubwa EPL zilivyo na ratiba
ngumu.
Manchester United, wametoka kucheza Jpili mchezo wa ligi zidi ya WBA
lakini kesho wako uwanjani mchezo wa Carbao Cup vs Bristol na siku tatu
baadae watwafuata Leicester City kisha siku tatu baadae watarudi
nyumbani kuisubiri Burnley na kisha Southampton tar 30, watapumzika tar
31 na ikifika tareh 1 watakwenda Goodison Park kuikabili Everton kabla
ya kucheza na Derby Country siku nne baadae.
Manchester City, hii leo watacheza vs Leicester City ugenini baadae
Jumamos watawakaribisha FC Bournamouth kabla ya kuwafuata Newcastle siku
tatu baadae kisha watapumzika na baada ya siku tatu Dec 31 watawakabili
Crystal Palace na watapumzika siku moja kisha tar 2 January watawaalika
Watford na Jan 6 watakuwa Etihad kuwakabili Burnley.
Chelsea, leo Dec 20 wanawakaribisha Fc Bournamouth kisha Dec 23
watawafuata Everton, Dec 26 watawakaribisha Brighton kisha Dec 30
watawakaribisha Stoke City baada ya hapo watapumzika siku 3 kabla ya
kucheza mchezo mgumu ugenini vs Arsenal na Jan 6 watamalizia na Norwich.
Arsenal, hii leo watacheza vs West Ham, na kisha siku ya Ijumaa
watawakabili Liverpool wakiwa nyumbani, Dec 28 watawafuata Crystal
Palace kisha siku ya mkesha wa mwaka mpya watacheza vs West Brom,
wataukaribisha mwaka tar 3 January vs Chelsea kabla ya Jan 7 kukipiga vs
Nottinghma Fores.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma iemwachia kwa dhamana aliyekuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis
(Mbunge) anayekabiliwa na mashtaka ya kutoa rushwa wakati wa uchaguzi
mkuu wa viongozi wa UVCCM Taifa.
Sadifa ameachiwa leo Desemba 19, 2017 baada ya mahakama kutupilia mbali
pingamizi la upande wa mashtaka ambao waliliwasilisha mahakamani hapo
kuweka zuio la kupewa dhamana.
Mtuhumiwa huyo ametakiwa kudhaminiwa na watu watatu pamoja na kusaini
bondi ya Tsh. Milioni 1, huku akipewa masharti ya kutosafiri nje ya
nchi.
Meneja wa wagonga nyundo wa London West Ham United David Moyes, amesema
uwezo alionao kwa sasa anaweza kuifundisha timu yoyote duniani na
anataka kuonesha kama ana uwezo huo akiwa na klabu yake ya West Ham
United.
Tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa West Ham United Moyes, ameisaidia
timu hiyo kutoka katika mstari wa timu zinazotakiwa kushuka daraja kwa
kutokufungwa michezo mitatu.
"Nina uwezo wa kufanya kazi hii katika klabu yoyote duniani na nina
uhakika nitalifanya hili nikiwa na West Ham," alisema kocha huyo.
Kocha huyo raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 54, anajaribu
kurudisha heshima yake baada ya kufanya vibaya alipoviongoza vilabu vya
Manchester United, Real Sociedad na Sunderland.
U
tawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa
moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki
kote duniani mapema mwaka huu.
Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.
Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya
kupitia jarida la Wall Street Journal, Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani
imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho.
Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa
nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.
Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya Microsof waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.
Rais Donald Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika
utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani.
Mkakati huo umesisitiza ukuaji wa kiuchumi na usalama wa taifa hilo kwa
kuweka sheria kali za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara.
Katika hotuba yake,rais Trump ametaja kuwa China na Urusi ni washindani
wanaopinga ushawishi wa Marekani katika ngazi ya kimataifa.
Licha ya kuwa Marekani inaongoza kwa kuwa na jeshi lenye nguvu lakini
bado wapinzani wake wa kisiasa na kiuchumi wanahangaika duniani kote ili
kuitoa katika mstari.
Huku ikiwa inakabiliwa na makundi ya kigaidi ,mitandao ya wahalifu na watu wengine ambao wanachochea vurugu na uovu.
Aidha mkakati huo unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico,
kuimarisha sheria za uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza za
bahati nasibu.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imekanusha
taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa wanamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu.
Akiongea na East Africa Television leo, Afisa habari wa TAKUKURU Musa
Misalaba amesema wanashangaa taarifa hizo zimetoka wapi na wao kama
taasisi hawamshikilii Mkurugenzi huyo aliyesimamishwa na Waziri Lukuvi
wiki iliyopita.
“Hizo taarifa sijui zimetoka wapi, lakini sisi hatuna huyo mtu,
hatujamkamata saa tunashindwa kuelewa watu wanazusha kwa lengo gani”,
amesema Misalaba.
Aidha msemaji huyo ameongeza kuwa wao kama taasisi hawajapokea agizo
lolote la kumkamata na kumfanyia uchunguzi ndugu Nehemia Mchechu hivyo
hawana sababu ya kumkamata.
Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es salaam leo ambapo imeamuachia huru
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa
iliyokatwa na Jamuhuri kupinga Hukumu ya Mahakama ya Morogoro
iliyomuachia huru Ponda.
Sheikh Ponda ameachiwa huru mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye
amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro kumuachia huru
Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.
“Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi
nakubaliana na uamuzi huo, hivyo namuachia huru,” – Jaji Mkasimongwa
Miongoni mwa hoja alizozitoa Jaji Mkasimongwa ni kwamba upande Jamhuri
haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya
Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili
imchukulie hatua zaidi.
Katika mashtaka yaliyokuwa yakimkabiri katika Mahakama ya Morogoro,
Sheikh Ponda anadaiwa August 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege,
Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na
BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Pia inadaiwa aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza
kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti,
wafunge milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa May 9, 2010, ambayo
ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Leo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema CCM kimekuwa
chama imara na chama kinachoendelea kuwavutia watu wengi kila siku
ikiwemo viongozi na wanachama kutoka vyama upinzani nchini.
Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na uimara wa CCM amepokea majina
nane ya madiwani wa vyama vya upinzani na Mbunge mmoja ambapo wanasubiri
muda tu kutangazwa.
“Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja
anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye
jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli
kweli.“amesema Rais Magufuli leo Desemba 18, 2017, kwenye Mkutano Mkuu
wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao unafanyika mjini Dodoma.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anaamini straika wake Zlatan
Ibrahimovic aliyerejea uwanjani hataweza kucheza vizuri kama ilivyo-kuwa
awali, hivyo yupo mbioni kumsajili Gareth Bale.
Kwa muda mrefu Mourinho amekuwa akihusishwa na mipango ya kumuhitaji
Bale kutoka Real Madrid ili akaongeze nguvu ya ushambuliaji katika
kikosi chake.
Habari kutoka Man United, zimeeleza kuwa Mourinho anataka kumfanya Bale
kuwa usajili muhimu katika usajili ujao wa Januari ili kuimarisha kikosi
chake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England.
Awali, ilionekana kama ni vigumu kwa Bale raia wa Wales kutua Man United
lakini sasa inaonekana Madrid inaelekea kuchoka kuwa na mshambuliaji
huyo ambaye ana majeraha ya mara kwa mara.
Licha ya kuonekana kuwa na nia ya kumuuza, Madrid imeweka dau la pauni
milioni 79 kwa Bale japokuwa awali Man United inadaiwa kuweka mkakati wa
kutolipa zaidi ya pauni milioni 65 ili kumsajili Bale.
Tottenham Hotspur inaonekana kutaka kuizidi kete Man United, lakini
mazungumzo ya mwanzoni mwa msimu huu kati ya Bale na Man United yanampa
nafasi Mourinho ya kumnasa mchezaji huyo.
Mourinho anaelezwa kuweka presha ya kumsajili Bale kwa kiasi ambacho
Madrid watakitaka huku akibaki na mbadala wa Antonie Griezmann wa
Atletico Madrid endapo ishu ya Bale ikibuma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema ataanza kampeni rasmi ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani
tarehe 21 ya mwezi huu kwa kupanda miti katika mji huo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha
rasmi mkoani Dodoma ambapo atakuwa akiishi na kufanya majukumu yake
ikiwa sehemu ya azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya Dodoma
Makamo Makuu ya Nchi.
Makamu wa Rais alitoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumrahisishia kuhamia
Dodoma pamoja na Waziri Mkuu .
“Tupo Dodoma na Tumehamia rasmi Dodoma, Mwaka mmoja na nusu sasa toka
tamko la kuhamia Dodoma limetolewa kuwa ile safari ya Kanani kwa upande
wangu leo imetimia”
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa aliielezea siku ya leo kuwa ni siku ya furaha kubwa kwa
Watanzania wote haswa wakazi wa Dodoma.
Waziri Mkuu alimuhakikishia Makamu wa Rais kuwa Dodoma ni nzuri, na wana
Dodoma wamefarijika sana na sekta za utoaji huduma za jamii
zimetanuliwa.
Waziri Mkuu alisema kuwa Dodoma ni rahisi kufikika na wananchi kutoka
kona zote za nchi yetu, hivyo fursa zipo nyingi kwa wananchi wa Dodoma
na wa mikoa ya jirani.
Waziri Mkuu alianisha barabara kadhaa ambazo zimekamilika kwa kiwango
cha lami na zinazorahisisha usafiri kufika Dodoma lakini pia
alizungumzia mradi wa reli mpya ya Standard Gauge ambayo itasaidia
usafiri kwa muda mfupi kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa
Mjini kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama
Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.
Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa
wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa
na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni
kuuza hadi utu wa wapiga kura.
Msigwa ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka
upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama
na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.
"Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu na magari yangu.
Sikuingia bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sabu kuna
hoja kuna agenda na kazi kama chama tunapigania. Mkome kabisa kunipigia
simu mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa
Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza
kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na
kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo
nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na
sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike
hadharani" I am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka
wazi
Aidha Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji
pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa
makampuni na kuongeza kwamba alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa
mwanasiasa na mbunge.