Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele),
kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi
kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya
Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo,
Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi,
Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya
kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili
kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa
watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote
Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi
wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam
leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka
Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo,
miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi
Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji
wataondolewa katika nyadhifa zao.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa
Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na
Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo
Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata
hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa
kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya
Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa
magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata.
Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote
Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la
Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba
yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi
hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji
pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha,
alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika
nyadhifa zao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto
waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga
(kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya
Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao
Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara,
uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es
Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment