Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo ameitaka Wizara ya Mifugo, Chakula na Ushirika kuacha kutoa vibali
vya kusafirisha mahindi nje ya nchi kwa wafanyabiashara wa hapa nchini
kwani Serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku usafirishwaji wa
mahindi hayo nje ili kulinda viwanda vya hapa nchini.
Mhe. Gambo alisema hayo jana
baada ya kutembelea maghala matatu ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula{NFRA} Kanda ya Arusha kujionea hali halisi ya uhifadhi wa
mahindi katika maghala hayo na kuskiliza changamoto zake na kukuta tani
6,620 za mahindi zilizoko kwa sasa.
Alisema serikali Mkoani Arusha
ilishapiga marufuku uuzwaji wa mahindi nje ya nchi lakini kuna baadhi ya
wafanyabiashara wamekamatwa na vyombo vya ulizni na usalama wakiwa na
vibali kutoka Wizarani vinavyowaruhusu kupeleka mahindi nchi jirani ya
Kenya hali inayowafanya watendaji wa serikali kushindwa kufanya kazi
kutokana na mkanganyiko huo.
Mkuu huyo alisema uamuzi wa
kupiga marufuku uuzwaji mahindi nje ulitolewa na serikali kuu na Mkoa
ulisimamia hilo kwa lengo la kuvilinda viwanda vya hapa nchini kwa
uzalishaji wa bidhaa hivyo na kunufaika na unga na pumba za mahindi
tofauti na ilivyo sasa.
Alisema kutokana na mkanganyiko
huo aliwaomba watendaji wa Wizara kuacha kutoa vibali kwa
wafanyabiashara kuuza mahindi nje ili kuwasaidia wenye viwanda vya
nafaka kuuza unga na pumba nje wenye kiwango ili nao waweze kupata faida
na nchi iweze kupata faida zaidi.
Mhe. Gambo alisema mbali ya hilo
pia serikali Mkoani Arusha imefanikiwa kuziba njia zote za panya
zilizokuwa zikitumika na wafanyabiashara kutorosha mahindi kwenda nchi
jirani ya Kenya na kusema kuwa hilo nalo linapaswa kuungwa mkono na
Wizara ili amri hiyo iweze kutekelezeka.
‘’Vibali vya Wizara kwa
wafanyabiashara kuuza mahindi nje vinatuchanganya sana na vinapingana na
amri yetu na nchi kwa ujumla na kutokana na hali hiyo tunaiomba wizara
iache kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi na wafanyabishara wa ndani ili
waweze kuuza unga badala ya mahindi kwani watanufaika zaidi’’alisema
Gambo
Naye Meneja wa NFRA Kanda ya
Arusha, Abdillah Nyangasa alikitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, alisema
kuwa zoezi la ununuzi lililoanza agosti 25 mwaka jana na kumalizika
novemba 30 mwaka huo huo malengo yalikuwa kununuwa mahindi tani 15,000
lakini walifanikiwa kununuwa mahindi tani 5,111 tu na hiyo ni kutokana
na ufinyu wa bajeti.
Nyangasa alisema changamoto
iliyowakabili katika kipindi cha ununuzi kipindi hicho ilikuwa
uzalishaji mdogo wa nafaka hususani mahindi ambo haukwenda sambasamba na
mahitaji au matumizi ya kukidhi nchi na hali hiyo ilichangia sana bei
ya mahindi au unga kupanda kwa kasi kubwa kwenye soko lake karibu nchi
zima.
Alisema changamoto nyingine ni
udhibiti mdogo wa soko la mahindi kwenye maeneo ya mipakani kwani
kumekuwa na njia nyingi zizizo rasmi maarufu kwa njia ya panya kwa mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro na mahindi mengi yamevuka kwenda nchini Kenya
kitu ambacho yangesaidia sana uhaba mkubwa wa chakula ulioko sasa endapo
yangedhibitiwa.
Meneja huyo alisema kutokana na
ununuzi mdogo wa mahindi Kanda ya Arusha NFRA makao makuu inaanga lia
uwezekano wa kuongeza akiba hiyo kwa kuhamisha sehemu ya akiba yake
kutoka katika kanda zake za Nyanda za Juu Kusini ambazo ununuzi wake
ulikuwa wa kuridhika kidogo.
No comments:
Post a Comment