Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospter Muhongo (wa tatu kushoto) na Waziri wa Nishati na
Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhandisi Irene Muloni (wanne
kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Hafla ya
Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa michoro ya mradi wa Bomba la Mafuta
Ghafi kutoka Uganda Hadi Bandari ya Tanga Tanzania mjini Kampala Uganda.
Waziri wa Nishati na Madini,
Prof. Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Uganda baada ya kuhudhuria Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu
wa Awali wa Michoro ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi
Bandari ya Tanga, Tanzania. Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa, Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi
Kapuulya Musomba na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Marwa Petro.
Waziri wa Nishati na Madini,
Prof. Sospeter Muhongo tarehe 9/1/2017 aliongoza Ujumbe wa Tanzania
jijini Kampala nchini Uganda katika hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa
Awali (Front End Engineering Design -FEED) wa mradi wa Bomba la
kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga, Tanzania.
Uzinduzi huo ulifanyika Makao
Makuu ya Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa nchi zote
mbili za Uganda na Tanzania, Makatibu Wakuu wa nchi zote mbili,
Wakurugenzi wa mashirika ya mafuta na gesi, Kampuni zilizogundua mafuta
nchini Uganda za Total (Ufaransa), CNOOC (China), TULLOW
(Uingereza), Kampuni ya Mafuta ya Uganda National Oil Co. (UNOC),
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wawakilishi wa vyombo
vya habari.
Wakati wa uzinduzi huo ilielezwa
kuwa, FEED ni moja ya hatua muhimu katika kuhakikisha mradi huo
unatekelezwa katika viwango vinavyozingatia usalama wa kimazingira na
ustawi wa jamii.
Vilevile, ilielezwa kuwa, hatua
hiyo itajumuisha pia upatikanaji wa njia ya gharama nafuu ya kupitisha
bomba la mafuta ambapo pia Wataalamu wa taaluma mbalimbali watahusika
katika kuhakikisha mradi huo unafuata viwango na ubora wa kimataifa.
Pia , imeelezwa kuwa bomba hilo
litakuwa la kwanza kwa urefu duniani kuwa bomba linalopashwa joto muda
wote kutokana na asili ya mafuta yanayosafirishwa.
Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa
ushirikiano wa Serikali za Uganda na Tanzania na pia
utahusisha kampuni za TOTAL, CNOOC na TULLOW
No comments:
Post a Comment