Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa Wilaya ya Karatu wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani humo.
Katika Kikao kingine Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(aliyesimama mbele) akizungumza na Wazee wa
Karatu pamoja na Viongozi wa Dini.
Mtaalamu wa Halmashauri ya
Karatu(kwanza kulia) akiwaandikisha Wananchi wa Kijiji cha Oldeani
waliojiunga na Mfuko wa afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa hadhara na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akichangia Fedha kwa ajili ya wazee 10 kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Karatu Theresia Mahongo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.
Mrisho Gambo wakati wa kikao cha viongozi wa dini pamoja na wazee wa
Karatu.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Serikali Mkoani Arusha imesema
busara ilipaswa kutumika zaidi katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri
Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake
Wilayani Karatu katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za
kuvuta maji Umbali wa Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.
Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu
aliagiza kusogezwa kwa mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji
cha bonde la Eyasi ambapo akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea
baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa
wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa
kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo kiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na
umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa Chakula haikuwa busara
kwa wananchikuchoma mashine hizo bila kujali mazao ambayo tayari
yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama zilizotumika kununua mashine
hizo.
Aliongeza kuwa wananchi hao
walienda mbali zaidi kwa kujichukulia sheria mikononi na kuharibu mali
mbalimbali ikiwemo nyumba za wamiliki wa mashine hizo hali iliyopeleka
kuleta hofu, usumbufu na sintofahamu kwa wananchi wa maeneo hayo.
“Vyombo vya ulizni na usalama vupo
kwanini wananchi hawa wasiende kuripoti tatizo hilo kwenye vyombo
vinavyohusika na badala yake wanaamua kujichukulia sheria Mkononi,
Kisheria hairuhusiwi kwa mtu yeyeote kuharibu mali ya mwananchi ilikua
ni lazima tuwachukulie hatua wote waliofaya uharibifu ule” Alisema
Gambo.
Mhe. Gambo aliongeza kuwa haikuwa
rahisi kwa wananchi wa Mang’ola kuamua kufanya zoezi lile pekeyao
inaonekana kuna viongozi wa Kisiasa ambao wako nyuma ya vurugu zile na
sisi kama Serikali tunaamini jukumu la kiongozi ni kuleta Amani na sio
uvunjifu wa Amani na ukienda kinyume sheria inafuata mkondo wake.
“Hivyo katika kudhibiti vurugu
zile wananchi wote na viongozi wao waliohusika kwa namna moja ama
nyingine kufanya uharibifu wa mashine na mali za wananchi tuliwakamata
na kuwapeleka Mahakama ili iwe fundisho katika maeneo mengine” Alisem
Gambo.
Kwa kuwa sasa wahusika wamekwisha
tambua makosa yao tunaweza kukaa pamoja na kuangalia namna gani bora ya
kutumia maji ya bodne hili bila kusababisha vurugu za aina yeyote ili
kila mtuamiji aweze kunufaika na maji ya bonde hilo.
Bonde hilo linatumiwa na wananchi
zaidi ya elf 20 wanaojishughulisha na shughuli za Kilimo cha mazao
mbalimbali kwa njia ya umwagiliaji hutegemea maji yanayotoka katika
Bonde la
No comments:
Post a Comment