Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB
Tanzania Godfrey Ndalahwa, akiongea na wanawake wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani
Dar es salaam.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya
Umma wa benki ya KCB Bi. Christine Manyenye akiongea na wanawake
wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na
benki hyo mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB
Tanzania Godfrey Ndalahwa akizungumza na baadhi ya wanawake
waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani
Dar es salaam.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na Benki ya KCB mkoani Dar es salaam.
Benki ya KCB Tanzania yatoa
mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI. Programu
hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo
yanayosababisha biashara yake ishindwe kuendelea. Programu hii itaongeza
ajira nchini kwa wanawake na hivyo biashara zao zitapanuka na kuwa na
uwezo wa kuajiri wengine. Mafunzo haya yataendeshwa na wataalamu kutoka
Tanzania Entrepreneurship and Competitiveness Center -TECC waliobobea
katika masuala ya kijasiriamali, kifedha na ushindani wa biashara
“Mpango huu ni endelevu na
tumepanga kufundisha wajasiriamali 315 nchi nzima. Leo tunafundisha
wajasiriamali 100 katika makundi mawili tofauti. Mafunzo haya ni bure
kabisa, KCB Bank itagharimia gharama zote. Tunachokihitaji kutoka kwao
ni mahudhurio ya siku zote tatu na usikivu wa hali ya juu.” Alisema
Godfrey Ndalahwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB.
Bw. Ndalahwa aliendelea kwa
kusema kuwa mafunzo hayo yatafanyika mikoa yote ambako benki ya KCB ina
matawi, Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na pia Zanzibar.
Na tunalenga wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ambao tayari
wanaendesha biashara lakini wanataka kuziimarisha zaidi. Lengo ni
kuwawezesha kudhibiti vipengele vya uzalishaji na mgawanyo wa mapato na
faida {control over factors of production and distribution of income and
benefits) lakini zaidi ni kuwawezesha kuyatawala maisha yao kiuchumi na
kijamii.
“Matatizo tunayotarajia kutatua
kutoka kwa wanawake wajasiriamali ni elimu ya kifedha, kufikia huduma za
kifedha, Ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria,
uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha
biashara endelevu, ukosefu wa mtaji na utaalamu wa kuanzisha biashara
kubwa” alisema.
Mkurugenzi aliongeza kwamba baada
ya mafunzo hayo benki itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa
watatu watakaotembelea bishara zao na hii ni kwa wale tu ambao
watahudhuria mafunzo ya siku tatu yote na kuonyesha nia ya
kubadilika/kuendelea kibiashara). Maafisa hao watakua ni afisa fedha,
afisa sheria na afisa masoko.
Alimaliza kwa kuwaambia wanawake wajasiriamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
No comments:
Post a Comment