Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada huku akiwahimiza
wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili kukabiliana na
mabadiliko tabia nchi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha masanza kona wilayani busega mara
baada ya kuwasili akitokea mkoani mwanza rais magufuli amewashukuru
wananchi kwa kumchagua oktoba 25 mwaka 2015 na kuahidi kutatua matatizo
yanayowakabili yakiwemo ya maji na umeme .
Aidha amesisitiza kutotoa chakula cha msaada kwa wananchi na kuwahimiza
kufanya kazi kwa bidii sambamba na kulima mazao yanayostahimili ukame
kama vile mtama ,viazi na ufuta.
Rais magufuli ameahidi kutafuta fedha kwaajili ya kukamilisha kilomita
50 kwa kiwango cha lami kutoka bariadi mjini hadi maswa baada ya
kukamilika kwa barabara ya lamadi bariadi yenye urefu wa km 72.8.
No comments:
Post a Comment