Monday, 31 October 2016
Kidato cha nne kuanza mitihani kesho
Jumla ya watahiniwa 408,442 wa kidato cha nne wanatarajia kuanza
mitihani ya kidato cha nne itakayoanza kesho, ikiwa ni idadi pungufu ya
waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Akizungumza na wanahabari leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani
Tanzania Dk Charles Msonde amesema mwaka jana kulikuwa na watahiniwa
448,382 waliofanya mitihani huo.
Dk Msonde amesema maandalizi yote ya mitihani hiyo itakayomalizika Novemba 18, mwaka huu yameshakamilika.
Amewataka wanafunzi, walimu na wasimamizi kujiepusha na udanganyifu wa
mitihani kwani baraza hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria,
ikiwamo kuwafutia matokeo.
Kifo cha muuza samaki chazua maandamano
Maelfu wa raia wa Morocco walifanya maandamano wikendi hii katika miji
kadhaa baada ya muuza samaki mmoja kukanyagwa hadi kufa na lori la
kubeba takataka alipokuwa akijaribu kuchukua samaki wake ambao alikuwa
amepokonywa na maafisa wa polisi.
Kifo cha Maouhcine Fikri katika mji wa kaskazini wa Al-Houciema siku ya
Ijumaa kilizua hasira kali miongoni mwa raia katika mitandao ya kijamii.
Kifo chake kinafananishwa na kile cha muuza matunda wa Tunisia mwaka 2010 ambacho kilisababisha maandamano makubwa.
Mfalme wa Morocco King Mohammed VI amewaagiza maafisa wake kutembelea familia ya Fikri.
Wizara ya maswala ya ndani pamoja na ile ya Haki zimeahidi kuanzisha uchunguzi.
Malinzi ameteuliwa CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Issa Hayatou ameteua Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa
miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati maalumu ya mageuzi ya muundo wa CAF
itakayokuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho,
imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, katika Kamati hiyo ikayoongozwa na Rais
Issa Hayatou mwenyewe, Malinzi ameteuliwa katika Kamati hiyo
iliyotangazwa leo Oktoba 30, 2016 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais Dkt John Pombe Magufuli alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi
Rais Dkt John Pombe Magufuli,
akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta
alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo
nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
(kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta
wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini
Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake,
Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta, alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini
Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya, Mh. Willam Ruto.
Wahariri waukubali Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari
Anitha Jonas – MAELEZO
Wahariri wa vyombo vya habari
wameukubali Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari baada ya kuusoma kwa
umakini nakuona namna gani utasaidia kuinua tasnia ya habari nchini.
Hayo yamebainishwa katika
mahojiano maalum kwa njia ya simu na baadhi ya wahariri wa vyombo vya
habari akiwemo Mhariri wa Televisheni ya TV 1, Bw.Said Mwishehe huku
akieleza faida za Muswada huo pamoja na kutoa maoni yake kwa kuiomba
serikali kuangalia vizuri baadhi ya vipengele na kama kipengele cha 54
na 55 katika Sehemu ya Nane ili kuvipunguzia makali na kuondoa suala la
kuonekana kubana uhuru wa vyombo vya habari.
“Kuna umuhimu kwa wadau wa habari
kuunga mkono muswada huu badala ya kuupinga kwani una mambo mazuri
yatakayosaidia kuboresha tasnia hii ya habari na kuipa heshima kama
taaluma nyingine badala ya kuonekana kuwa waandishi wa habari ni watu
wababaishaji tu na wasiyo na taaluma iliyo imara,”alisema Bw.Mwishehe.
Pamoja na hayo Mhariri huyo
aliendelea kusema amefurahishwa na muswada kwa namna unavyojali maslahi
ya waandishi wa habari pale unapoeleza kuwa wamiliki wa vyombo vya
habari watahitajika kuwakatia bima waandishi wa habari kwa hiyo itakuwa
jambo la busara kwani waandishi wamekuwa wakifanya kazi katika
mazingira magumu yanayohatarisha afya zao pasipo kuwa na bima
inayomlinda akiwa kazini.
Aidha, Bw.Mwishehe aliwasihi
wadau wa sekta ya habari kutuma maoni yao kwa vile vipengele vya muswada
vinavyoonyesha kutokuwa sawa na pia ameiomba serikali kuwa na utayari
wa kuyapokea maoni hayo kwa ajjili ya kuboresha muswada huo na kuufanya
bora na wenye tija katika tasnia ya habari nchini.
Naye Mhariri wa Gazeti la
Mtanzania, Bw.Revocatus Makaranga alisema Muswada huo wa habari una
mambo mazuri yanayoipeleka tasnia mahali pazuri ikiwemo suala la
waandishi wa habari kuhitajika kujiendeleza katika elimu ya juu na hii
itasaidia kukuza upeo wa mwandishi na kumfanya awe na uwezo mkubwa na
kufanya kazi kwa kujiamini kama ilivyo kwa waandishi wa nchi
zilizoendelea.
Bw.Makaranga aliongeza kusema
muswada una vipengele ambavyo ipo haja ya serikali kuvifanyia
marekebisho ikiwemo suala la adhabu inayotolewa kwa waandishi ya
kuwafungia pale wanapokuwa wamekosea.
Pia mhariri huyo ameipongeza
serikali kwa muswada huo ambao utaleta picha mpya ya kimaendeleo katika
tasnia ya habari ikiwemo suala la kuanzishwa kwa Mfuko wa mafunzo kwa
wanahabari nchini ambapo utasaidia kutoa elimu kwa waandishi mara kwa
mara na kuwajengea uwezo wa utendaji.
Kwa upande wake, Mhariri Mkuu wa
kituo cha Redio Efm, Bi Scolastika Mazula alisema katika muswada huo wa
habari yapo mambo mazuri yenye tija katika sekta ya habari kama suala la
kuanzishwa kwa Mfuko wa mafunzo kwa wanahabari ni jambo jema sana kwani
utasaidia kutoa fursa za waandishi kujiendeleza kimasomo na kuifanya
fani ya habari kuwa na wasomi zaidi tofauti na inavyoonekana kwa sasa.
“Suala la elimu kwa waandishi ni
bora liwekwe wazi kisheria kwani tansnia hii ya habari inahitajika
kuheshimika kama ilivyo tansia nyingine badala ya kuonekana
wababaishaji”, alisema Mazula.
Pamoja na hayo Bi. Mazula
aliendelea kutoa maoni yake kuhusu Muswada kwa kusema kuwa suala la
kuanzishwa kwa bodi ni zuri ila ingekuwa vyema kama bodi hiyo itakuwa na
asilimia kubwa ya wadau wa habari na ijitegemee na Waziri mwenye
dhamana ya habari na Mwanasheria Mkuu wasiwe na mamlaka sana katika bodi
hiyo.
Pamoja na hayo naye Katibu wa
Jukwaa la Wahariri, Bw.Neville Meena alisema kwa sasa wanajukwaa
wameshatoa maoni yao kuhusu muswada huo na watayawasilisha kwa ajili ya
kusaidia kuboresha muswada huo na kuufanya uwe na tija na manufaa zaidi
katika kuendeleza tasnia ya habari nchini.
Alichokisema Jokate kuhusu shindano la Miss Tanzania
Kwa miaka mingi mfululizo, haijawa rahisi kwa shindano la Miss Tanzania
kumalizika bila malalamiko, lawama au kashfa. Awamu hii pia, yamekuwepo
malalamiko kadhaa kuhusiana na maandalizi yake na jinsi shindano
lilivyofanyika huku kukiwepo kasoro kadhaa.
Lakini mrembo aliyewahi kushiriki shindano hilo miaka ya nyuma, Jokate
Mwegelo, ameyatetea mashindano hayo akisema kuwa waandaji wamefanya kazi
nzuri na wanastahili pongezi. Haya ni maelezo yake aliyoandika kupitia
Twitter.
Fainali za mashindano ya Miss Tanzania zitafanyika Mwanza kwa miaka
mitatu zaidi. Brilliant idea. I support this move. Open up mikoa zaidi.
Ukiacha mapungufu fainali za Miss Tz ni shindano pekee la urembo ambalo
huwezi kusikia mshindi amedhulumiwa zawadi yake au show ikapwaya.
Show ya Mwanza ilifanyika nje viingilio 100k,50k,20k na ilijaa watu
licha ya mapungufu ya production. Nilikuwepo so najua ninachoongea.
Wadada wawili walipewa jukumu la kusimamia fainali hizi. Hao wadada
wanakaa mkoani Mwanza. Nawapongeza kwa kufanikisha licha ya changamoto.
Kamati just needs to perfect the craft of moulding contestants to be
competitive and of coarse giving us the ideal winner who will thrive. Ni
rahisi sana kuchambua na kukosoa mashindano haya humu ila ukilinganisha
na mashindano mengine ya urembo nchini angalau wanafanya vizuri.
Wanafanya vizuri kufikia warembo wengi kupitia mikoa mbalimbali na
sio DSM tu au mikoa ya karibu. Vipaji vinatoka sehemu mbalimbali.
We need a sole company to deal na production. Creative themes and
execution. Sio tu kwenye show za urembo na kwenye matamasha mengine.
Mshindi wa Miss Tanzania mwaka huu ni Diana Edward.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 utanufaisha waandishi wa habari?
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya
Mawasiliano Serikalini (GCU) wamemesema Muswada wa Sheria ya Huduma za
Habari wa mwaka 2016 ni muhimu kwa taifa na unalenga kuleta tija kwa
taifa zima.
Muswada huo unalenga kuwanufaisha waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wananchi wa kawaida nchini.
Wakipongea kwa nyakati tofauti na
mwandishi wa habari hii, Wakuu hao leo wa wamesema muswada huo una
manufaa na fursa nyingi kwa taifa na wananchi tofauti na hali ilivyokuwa
hapo awali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla amesema
kuwa sheria hiyo inatoa mwanya mkubwa kwa tasnia ya habari nchini kuwa
ni miongoni mwa taaluma inayoheshimika kama kada nyingine kwa kuwa na
chombo kitakachowasimamia wanahabari hao.
“Uanzishwaji wa Baraza Huru la
Habari ni moja ya takwa lililowekwa na Sera ya habari na Utangazaji ya
mwaka 2003 iliyoitaka Serikali kuanzisha chombo huru kitakachosimamia
masuala ya habari hivyo,muswada huu utakapokuwa sheria utakuwa
umetekeleza agizo la Serikali la kuanzisha chombo huru kitakachosimamia
masuala ya habari”, alisema Msalla.
Zawadi ameongeza kuwa kuanzishwa
kwa Sheria hiyo itasaidia kuleta uhuru wa vyombo vya habari na
wanahabari kufanya kazi yao ipasavyo kwani kwa sasa mmiliki wa chombo
cha habari asiporidhishwa na maamuzi ya kutopewa leseni anakata rufaa
kwa Waziri mwenye dhamana na asiporidhishwa na maamuzi yaliyotolewa na
Waziri huyo amepewa fursa ya kwenda mahakamani.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Morogoro, Andrew Chimesela amepongeza
juhudi za Serikali kwa kazi ya kuandaa Muswada ambao utasaidia kuwa na
Sheria itawanufaisha wadau wote wa habari nchini.
Baada ya kupitishwa Muswada na
Bunge, kuidhinishwa na kusainiwa na Rais hatimaye kuwa Sheria, Chimesela
kuwa ziandaliwe kanuni ambazo zinaendana na wakati huu wa sasa tofauti
na ilivyokuwa wakati wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Aidha, amekubaliana na uamuzi wa
kuundwa kwa Bodi ya Ithibati kwa sababu bodi hiyo itakua na kazi ya
kuangalia maslahi ya wanatasnia pamoja na kudhibiti nidhamu na maadili
ambayo yanapaswa kwenda sambamba na tasnia habari ili iweze kuheshimika
kama taaluma nyingine za Wanasheria, wahasibu na sekta ya afya.
Naye Mkuu wa Kitengo cha GCU
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Englibert Kayombo na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
wameunga mkono uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati kwasababu itasaidia
kutambua wanahabari wenye taaluma halali kwenye sekta ya habari nchini.
“Binafsi naunga mkono jitihada
zinazofanywa na Wizara za kurasimisha tasnia hii ya habari ili iwe na
hadhi sawa na tasnia zingine, ni vyema kuratibu kazi za waandishi wa
habari ili waweze kutoa habari zenye kujenga taifa letu imara lenye
mfumo mzuri wa kazi za kihabari”, alisema Kayombo.
Baada ya kuanzishwa na kufanya
kazi Sheria hiyo, ni dhahiri itavifanya vyombo vya habari nchini kuajiri
watu wenye taaluma ya habari tofauti na hali ilivyosasa na wananchi
watarajie kupata habari za ukweli na uhakika.
Kitabu cha Timiza malengo yako chazinduliwa
Imeelezwa kwamba watu wengi
wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa na mipango
ya kimaisha ambayo wanaweza kuifanyia kazi ili waweze kufanikiwa kama
jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wanaonekana kuwa na mafanikio.
Hayo yamesemwa na Mwandishi wa
kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka wakati wa uzinduzi wa
kitabu hcho ambacho kinnaelezea mbinu 60 ambazo zinatumiwa na watu
waliofanikiwa kimaisha kuweza kufikia alengo ambayo wamejiwekeakatika
maisha yao.
Nanauka alisema watu wengi
wamekuwa wakitamani kufanikiwa lakini wamekuwa hawajui ni hatua gani za
kupitia na kufanikiwa na baada ya yeye kufanya utafiti wa muda mrefu kwa
watu mbalimbali duniani waliofanikiwa na wasiofanikiwa, ameweza kupata
mbinu 60 ambazo ndiyo zinatofautisha watu wa matabaka hayo mawili
Alisema kupitia kitabu hicho
msmaji ataweza kufahamu ni mambo gani anatakiwa kufanya na yapi hatakiwi
kufanya ili kufanikiwa kama wengine kwa kuzingatia mbinu ambazo pia
zimekuwa zikitumiwa na watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kama
biashara, michezo, sanaa na hata uongozi.
“Watu wengi wanapenda kufanikiwa
lakini kama huna malengo huwezi kufanikiwa, watu wengi hawajui wanatumia
njia gani ili kufanikiwa na hadi wanaondoka duniani wanaondoka na ndoto
walizokuwa nazo, ndoto ambazo zilitakiwa kubaki zikifanya kazi duniani,
“Sababu ya kuandika kitabu hiki
ilianza nipotaka kujua utofauti wa waliofanikiwa na wasiofanikiwa,
aliyefanikiwa kwa aliye Marekani na Tanzania na asiefanikiwa aliye
Tanzania a Mareani, nilianza kusoa kwanini wengine wanaweza kufanikiwa
katikati ya mamilioni ya watu na baada ya kupata mawazo ya jumla ndiyo
nikapata mbinu 60 ambazo zipo katika kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO,”
alisema Nanauka.
Nanauka alisema kitabu hicho
kitakuwa kikuzwa kwa Tsh. 10,000 na anaamini kila ambaye ataweza kusoma
kitabu hicho ataweza kupata kitu kipya ambacho kitaweza
kumsadiakufanikiwa na kufika ndoto abazo anatamani kuzifikia.
“Matumaini yangu kila atakaesoma
kitabu hiki maisha yake yabadilike kutokana na mambo ambayo atayasoma na
kila mtu hatajutia kusoma kitabu hiki, nimekiandaa kwa muda mrefu kwa
kufanya tafiti nyingi na kuweka mifano ambayo naamini itabadili maisha
ya watu wengi wataokisoma,” alisema Nanauka.
Ziara ya Rais Dkt John Pombe Magufuli nchini Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya
kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa Kenya
nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya
kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta
jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi,
Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya
kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wakati akipanda ndege kwenye
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya
kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba
31, 2016
Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga
mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati
akianza safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku
mbili leo Oktoba 31, 2016
Rambo alivyomuibukia Pacquiao Gym
Bondia
Mfilipino, Manny Pacquiao akiwa na gwiji wa filamu za kibabe Marekani,
Sylvester Stallone maarufu kama Rambo au 'Bondia Rocky' mjini Las Vegas,
Marekani. Pacquiao yupo katika maandilizi ya mwisho na pambano na
Jessie Vargas Novemba 5 mjini Las Vegas uzito wa Welter na mwishoni mwa
wiki alitembelewa na Rambo katika gym ya Wild Card mjini Hollywood
Alikiba, Diamond, Ommy wakutana kwenye kipengele kimoja Tuzo za ASFA 2016
Waandaaji wa tuzo za mitindo za Uganda, Abryanz Style and Fashion Awards
wametangaza majina ya mastaa watakaowania vipengele mbalimbali.
Wakali wa muziki wa Afrika mashariki, Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz na
Sauti sol wamekutana kwenye kipengele kimoja cha ‘Most stylish artiste’
Huku Juma Jux, Nedy Music na Idris Sultan wakikutana kwenye ‘Male Most
dressed Celebrity’
Jokate Mwegelo, Wema Sepatu na Wolper Stylish watachuana na Vera Sidika,
Huddah Monroe na Kate Peyton kweney ‘Female Most dressed Celebrity’
Hii ndio orodha kamili ya Nominees,
FASHION DESIGNER OF THE YEAR
Martin Kadinda (Tanzania)
Sheria Ngowi (Tanzania)
Bobbins & Seif (Uganda)
Moise Turahirwa (Rwanda)
Makeke International (Tanzania)
Jamila Vera Swai (Tanzania)
MOST STYLISH ARTISTE
Males
Sauti Sol (Kenya)
Ali Kiba (Tanzania)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Ommy Dimpoz (Tanzania)
Females
Vanessa Mdee (Tanzania)
Avril (Kenya)
Vicotria Kimani (Kenya)
Aika Navy kenzo(Tanzania)
BEST DRESSED CELEBRITY
Males
Nick Mutuma(Kenya)
Juma Jux(Tanzania)
Nedy Music(Tanzania)
Idris Sultan(Tanzania)
Georgie Ndirangu(Rwanda)
Jamal Gaddafi(Kenya)
Females
Jokate Mwegelo(Tanzania)
Vera Sidika(Kenya)
Huddah Monroe(Kenya)
Wema Sepatu(Tanzania)
Kate Peyton (Rwanda)
Wolper Stylish(Tanzania)
MOST FASHIONABLE MUSIC VIDEO
Mamacita – Tinie Tempah ft. Wizkid
Colours of Africa – Diamond Platnumz ft. Mafikizolo
Soft Work – Falz the bahd Guy
Vanessa Mdee – Niroge
No Kissing – Patoranking ft. Sakordie
Aje – Ali Kiba
If I start to talk – Tiwa Savage ft. Dr. SID
Tulale Fofofo – Micasa FT. Sauti Sol
Kontrol – Maleek Berry.
MOST STYLISH COUPLE
Barbie and Bobi Wine (Uganda)
Bonang Matheba & AKA (South Africa)
Annabel Onyango and Marek Fuchs (Kenya)
Zari Tlale and Diamond Platnumz(Tanzania)
Mr & Mrs Ayo Makun(Nigeria)
Elikem and Pokello(Zimbabwe)
CROSSING BOARDERS WITH FASHION
Jidenna
Ugo Mozie
Lupita Nyongo
LOLU ESQ
BEST DRESSED MEDIA PERSONALITY/ENTERTAINERS OF THE YEAR(AFRICA)
Males
Uti Nwachukwu
Falz the bahd Guy
Idris Sultan
Friday James
Ebuka Obi
Derenel Edun
Georgie Ndirangu(Rwanda)
Females
Vimbai Mutinhri
Toke Makinwa
Stephanie Coker
Bolanle Olukanni
Berla Mundi
Bonang Matheba(SouthAfrica)
Tracy Wanjiru(Kenya)
Bondia Thomas Mashali auwawa, mwili wake waokotwa vichakani Dar
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.
Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa
mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam.
"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
Sunday, 30 October 2016
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Taasisi ya Twaweza wameunga mkono Mswada wa Huduma za Habari ya mwaka 2016
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS) na Taasisi ya Twaweza wamesema kuwa Muswaada wa Sheria ya Huduma
za Habari ya mwaka 2016 ni bora kuliko Miswada iliyowahi kuwasilishwa
nchini.
Haya yamebainishwa katika maoni
yao waliyowasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii leo Mjini Dodoma katika juhudi za kuufanya Muswada huo kuwa bora
zaidi na kupelekea kuapa sheria yenye tija kwa wananchi na taifa kwa
ujumla.
TLS na Twaweza wamebainisha kuwa
Muswada huu ni bora zaidi na utasaidia kuwajengea wadau wa habari
nchini heshima kwa kutoa huduma bora kupitia vyombo vya habari kwa
kuzingatia taaluma ya Habari waliyonayo hatua ambayo inautofautisha na
muswada uliowasilishwa Bungeni mwaka 2015.
Kwa mujibu wa maoni yalitolewa na
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) yamesema Muswada huo mzuri zaidi
na unaifuta Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 hatua ambayo wameipongeza
Serikali kwani Sheria hiyo iliwahi kuainishwa kuwa miongoni mwa Sheria
40 na kusadikiwa na Tume ya Jaji Francis Nyalali kama Sheria kandamizi.
Kwa upande wa Taasisi ya Twaweza
wao wamesema kuwa Muswada huo utaanzisha utaratibu ambao utawatambua
waandishi wa habari kwa kuanzisha Baraza Huru la Habari pamoja na Bodi
ya Ithibati ya wanahabari amabazo zitasimamia kanuni na maadili ya
wanahabari, kusimamia viwango na mienendo ya kitaaluma na kuendeleza
vigezo bora vya maadili na nidhamu miongoni mwa wanahabari.
Kwa mantiki hiyo, maoni
yaliyowasilishwa kwa Kamati hiyo yanaendana na Muswada ambao unasisitiza
kuanzisha mahusiano na taasisi nyingine za taaluma ya habari ndani na
nje ya nchi ili wadau wa habari waweze kubadilishana mawazo na kuwa na
namna bora ya kuhabarisha umma katika masuala mbalimbali ya kijamii na
kiuchumi.
Aidha, Baraza huru la habari
kutakuwa suluhisho katika kusimamia na kusikiliza malalamiko ambayo
yatawasilishwa kwenye baraza hilo kulingana na kanuni za maadili ya
taaluma ya habari hatimaye kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofauti
na hali ilivyokuwa hapo awali.
Uboreshwaji wa Muswada huo
unalenga kuleta Sheria itakayosimamia Tasnia ya Habari ili iweze
kuendana na wakati pamoja na Sheria za kimataifa na namna bora ya
kuwahudumia wananchi.
Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Rais wa Jamhuri ya Muunganowa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua
Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika
la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.
Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.
WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli
amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy
Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya
Ng’ombe Makao Makuu ya TALIRI.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Oktoba, 2016
Italia yagongwa tena na tetemeko la ardhi
Taarifa za awali zinasema kuwa uzito wa tetemeko hilo limefikia 6.6 katika vipimo vya Richa.
Majumba kadhaa yameporomoka, likiwemo kanisa la St Benedict mjini Norcia.
Hakuna taarifa zozote kuwahusu wahasiriwa au maafa.
Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia.
Uzito wa tetemeko hilo umesikika hadi mjini Roma, umbali wa kilomita 150.
Pluijm Kwenye Benchi La Yanga Leo Tena
Pluijm raia wa Uholanzi aliamua kuandika barua kuachia ngazi, lakini uongozi wa Yanga ukamuangukia na kumfanya abadili uamuzi wake huo.
Leo Yanga inapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mechi ya kwanza baada ya Pluijm kurejea.
"Najua itakuwa mechi ngumu, timu zote zinajiandaa na inakuwa faraja kwao kushinda dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa.
"Wachezaji wangu wako tayari na wanajua sisi ni kina nani na wanaocheza na sisi wanataka nini," alisema.
Yanga imeonyesha kurejea katika kiwango chake kwa kushinda mabao mengi katika kila mechi, ikianza na kuitandika Kagera Sugar mabao 6-2 na JKT Ruvu mabao 4-0.
Sumaye adai Amepata taarifa ya Kutimuliwa Nyumbani kwake pia
Sumaye ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa kumnyang’anya mwanasiasa huyo shamba la Mwabwepande kwa madai ya kutoliendeleza kwa muda mrefu.
“Hapa ninapoishi naambiwa kuna maelekezo yametoka juu kuwa sijapaendeleza. Sasa kama sijapaendeleza mbona ninaishi hapahapa,”
Aidha Sumaye amesema kuwa ingawa alimsikia Waziri Lukuvi akieleza kuwa tayari wameshampa notisi ya siku 90 kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Mwambwepande, hadi jana hajaipata notisi hiyo licha ya kufanya jitihada za kuifuatilia.
Alisema kuwa anashangazwa na uamuzi huo wa Waziri kwani kesi inayolihusu shamba hilo bado inaendelea mahakamani kutokana na uvamizi wa wananchi na kwamba Mahakama imezitaka pande zote mbili kutofanya chochote kwenye ardhi hiyo.
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema alisema kuwa anachokifahamu ni kwamba alipokea notisi ya kuondolewa katika shamba lake la Mvomelo kwa madai ya kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu.
“Ninachokijua ninaandamwa kisiasa. Shamba langu la Mvumelo naambiwa sijaliendeleza. Kwenye hilo shamba nimejenga nyumba ya kuishi, ghala, kuna trekta na vifaa vingine. Ninalima mazao na nimefuga zaidi ya ng’ombe 200, nina kondoo 300 na nimechimba visima viwili vya maji halafu serikali inasema sijaliendeleza,” alisema Sumaye.
Alisisitiza kuwa ingawa anaamini anaandamwa kisiasa kwa kunyang’anywa mashamba yake, hatarejea CCM hata akinyang’anywa mashamba yote aliyoanayo.
Sumaye alihama CCM mwaka jana, miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu na kujiunga na harakati za kumpigia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa. Baada ya uchaguzi huo alitangaza kujiunga rasmi na Chadema.
Samatta Atokea Benchi Genk Ikiua 2-1 Ubelgiji
Kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo aliifungia bao la kwanza Genk dakika ya 54 kabla ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis kufunga la pili dakika ya 66, wote wakimalizia pasi za mshambuliaji Mjamaica, Leon Bailey.
Na ni Nikolaos Karelis aliyempisha Samatta, Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dakika ya 66 mara tu baada ya kufunga bao la pili. Bao pekee la wageni lilifungwa na kiungo Mbelgiji, Jamo Molenberghs dakika ya 82.
Huo unakuwa mchezo wa 31 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 12 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika mechi hizo, ni 16 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 14 alitokea benchi nane msimu uliopita na 11 msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Saturday, 29 October 2016
ACT wamjibu Ole-Sendeka
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa ya ACT, Habib Mchange alisema chama hicho hakina shaka kwamba kiongozi wake ni msafi.
"Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja na tutafurahi ukihusisha pia akaunti zake binafsi "alisema Mchange
9 wauawa katika shambulio Maiduguri Nigeria
Inaarifiwa kuwa washambuliaji hao walizunguka mjini ndani ya bajaji.
Mlipuko wa kwanza ulitokea wakati walipuaji wawili wa kujitoa muhanga walipojaribu kuingia katika kambi - ambayo maelfu ya watu wanaishi baada ya kulazimika kuyatoroka makaazi yao kufuatia kuzuka uasi.
Jamaa mmoja aliyeshuhudia mkasa huo ameeleza kuona watu waliojeruhiwa wakivuja damu.
Muda mfupi baadaye kumetokea mlipuko wa pili karibu na ghala la mafuta.
Jeshi la Nigeria limepiga hatua kubwa katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.
Lakini wanamgambo hao wa kiislamu bado ni tishio na hutekeleza mashambulio ya kujitoa muhanga kila mara.
Ndege yashika moto ikipaa
Viongozi wa ndege hiyo wanasema kuwa abiria saba na mhudumu mmoja walijeruhiwa lakini walikimbizwa hospitali kwa uchunguzi.
Hata hivyo baadaye uongozi wa ndege hiyo ulisema kuwa watu zaidi ya 20 walikimbizwa
Guardiola arusha kijembe cha chini chini kwa Man United kwa matumizi ya mipira mirefu
Guardiola leo atakuwa na kibarua kigumu mbele ya West Brom kwenye dimba la Hawthorns, mchezo ambao utakuwa mgumu kwake kufuatia kucheza michezo sita mfululizo bila ushindi, rekodi ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake ya ukocha.
Man City walifungwa bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Man United katika Uwanja wa Old Trafford katikati ya wiki hii kwenye mchezo wa Kombe la EFL.
“Goli tulilofungwa katika mchezo dhidi ya United lilitokana na mpira mrefu, tukashindwa kuudhibiti na hatimaye tukafungwa.
“Wakati mwingine unaruhusu goli kwasababu umeshindwa kuzuia mipango ya goli kama ilivyotokea kwetu na wakati mwingine unaweza kutumia pasi ndefu na ukaruhusu goli vile vile.
Guardiola alienda mbali zaidi kwa kusema: “Kwa aina ya washambuliaji tulio nao kama Kelechi, Kun Aguero, si vyema kwangu kutumia pasi ndefu, labda kwa siku zijazo nikinunua straika mwenye urefu wa sentimeta 220 nitaweza kutumia mfumo huo.
Rais Dkt Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mkurugenzi Wa Upelelezi Makosa Ya Jinai (Dci) Diwani Athumani Leo
Taarifa kutokea Ikulu Dar es salaam leo October 29 2016 ni pamoja na hii
ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa mkurugenzi wa Makosa
ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani.
Mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry kumaliza mgogoro wa beki Hassan Ramadhani Kessy
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry
anatarajia kuwakutanisha viongozi wa Simba na Yanga ili kumaliza utata
wa beki Hassan Ramadhani Kessy na kuotoa mgogoro uliopo katika usajili
kwa pande zote mbili.
El
Maamry anakutana na pande hizo mbili kujadili suala la beki Hassan
Kessy ambaye Simba inamlalamikia kusajili na Yanga huku akijua ana
mkataba na wana msimbazi na Kessy anailalamikiwa Simba.
“Kweli
El Maamry amekubali na leo, ndiyo tunakutana kwa ajili ya kulimaliza
suala hilo na Simba,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga kutoka makao
makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Lengo letu ni kulimaliza hili suala, kwa kuwa hii nafasi
ya El Maamry ni nzuri kwa maana hiyo ya kulimaliza, tunaamini tutafikia
mwafaka na kumuacha mchezaji akili yake awaze mpira tu na sio mambo
mengine.
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambayo inashughulikia suala
hilo, ilitoa nafasi kwa Yanga na Simba kufikia mwafaka kabla yenyewe
haijatoa maamuzi.
Lakini
kama Yanga itashindwa na kuamliwa kulipa, itakuwa tatizo kwao kwa kuwa
tayari imeshamtumia Kessy katika mechi kadhaa za ligi kwa upande
mwingine msemaji wa TFF alishawahi kusema kuwa ishu ya Kessy sio usajili
na kuwaondoa mashabiki wa Yanga kuwa hawawezi kukatwa pointi zozote
kwani usajili wake ulipitishwa.
Beki huyu ameingia matatani na klabu yake ya zamani yaani
Simba kwa madai kuwa alivunja mkataba na kujiunga na Yanga huku akijua
kabisa ni kosa hivyo kamati itatoa uamuzi sahihi na sio wa kukomoana
hekima na busara zitatumika kumaliza suala hilo ambalo limekuwa ngumzo
kwa wadau.
Baada ya kamati hiyo kukaa na
kupata maamuzi, iliona inawezekana pia Yanga na Simba kukutana na
kulimaliza suala hilo badala ya kutoa maamuzi ambayo yatakuwa yanauumiza
upande mmoja
Mariah Carey anataka alipwe mamilioni na ex wake bilionea
Wawili hao waliachana baada ya kuzuka ugomvi walipokuwa wakila bata kwenye yacht nchini Ugiriki mwezi September kufuatia tetesi kuwa diva huyo anachepuka na dancer wake, Bryan Tanaka.
Kwa mujibu wa ripoti, Carey anataka alipwe dola milioni 50 kutoka kwa Packer baada ya kumhamishia LA na anadai kuwa ameathirika na kuachana kwao kiasi cha kukatisha ziara yake ya Amerika Kusini.
Hata hivyo vyanzo vilivyo karibu na bilionea huyo vimedai kuwa Carey asahau kupewa hata senti. “Ni ujinga kudai kuwa James ni sababu ya kusitisha ziara yake ya Amerika Kusini. Siku chache zilizopita aliwalaumu mapromota,” kilisema chanzo.
Sababu kubwa inayoelezwa kuwa chanzo cha wawili hao kuachana ni usaliti wa Carey na matumizi makubwa ya fedha. Wawakilishi wa muimbaji huyo wanakanusha.
Rais Magufuli atimiza miaka 57 awashukuru wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli leo Oktoba 29, 2016 anasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
ambapo anatimiza miaka 57.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘twitter’ Rais Dkt.
Magufuli amewashukuru watanzania wote kwa kumtakia heri na kuahidi
kuendelea kuchapa kazi kwa maslahi ya taifa.“Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea , nitafanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote” Amesema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Dkt. Magufuli anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ikiwa anakaribia kutimiza mwaka mmoja tangu alipoapa kuliongoza taifa la Tanzania Novemba 5, 2015.
Rais Dkt. Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 katika Wilaya ya Chato ambayo ni mojawapo ya wilaya tano za mkoa mpya wa Geita uliopo kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Wilaya ya Chato ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na ni mwaka 2012 tu ndipo ilipohamishiwa Mkoa wa Geita.
Kamati leo kupokea maoni ya wadau wa habari
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba
Wadau hao, waliotakiwa kutoa maoni yao tangu wiki iliyopita mbele ya kamati hiyo, waligoma kutoa kwa madai kuwa walipatiwa taarifa za kuwasilisha maoni yao kwenye kamati hiyo katika kipindi kifupi hivyo hawakujiandaa vyema.
Wadau waliohudhuria kikao hicho na kuomba kuongezewa muda ni Jukwaa la Wahariri (TEF), klabu mbalimbali za waandishi wa habari, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), MISATan, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika kikao hicho, wadau hao waliomba kuongezewa muda wa takribani miezi minne ili waweze kushirikisha wadau wengi zaidi kuupitia muswada huo na kutoa maoni yao kwa mrengo mmoja.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, aliongeza siku tisa ili wadau hao wajiandae kutoa maoni yao kwa ajili ya kuboresha muswada huo akibainisha kuwa muda uliotolewa kwa wadau hao tangu awali ulikuwa unatosha.
Mwenyekiti huyo alisema kamati hiyo haitaweza kukamilisha kazi yake ya kupitia na kuboresha muswada huo bila kupata maoni ya wadau ambayo nayo yatasaidia kuuboresha zaidi muswada huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano jana, kamati hiyo imepanga kupokea maoni ya wadau hao mjini Dodoma.
Mechi za ligi daraja la kwanza msimu wa 2016/2017 kuendelea leo
Katika kundi A kutakuwa na michezo miwili ambako Polisi Dar itacheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam wakati Friends Rangers itasafieri hadi Tanga kupambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ya kundi hilo ambako Mshikamano na Ashanti zitachuana jijini Dar es Salaam kwenye kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini.
Kundi B kutakuwa na michezo mitatu kwa siku ya leo Oktoba 29, 2016 ambako Mlale itaikaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Kurugenzi ya Mafinga itakuwa mwenyeji wa Kemondo ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uwambi huko Iringa ilhali Njombe Mji itacheza na Mbeya Warriors ya Mbeya huko Makambako.
Katika kundi hilo, KMC ya Dar es Salaam itacheza Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Kadhalika Kundi C kutakuwa na mechi tatu. Mechi hizi ni kati ya Singida United itayocheza na Polisi Mara kwenye dimba la Namfua mjini humo wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Polisi itakuwa mwenyeji wa Rhino ya Tabora ilhali Panone ya Kilimanjaro itacheza na Mgambo JKT ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushisirika mjini Moshi.
Tony Pulis amesaini mkataba mpya wakuendelea kuifundisha West Brom
Jeshi la Nigeria Lawaachilia Watoto 876
Watoto hao wamekuwa wakizuiliwa katika kambi za kijeshi kwenye mji wa Maiduguri ulio Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo makundi ya kibinadamu yanalalamika kuwa hakuna sheria ya kuwafungulia mashtaka watu hao.
Baadhi yao hupelekwa kwa vituo vya kurekebisha tabia ambavyo makundi ya kibinadamu yanasema kuwa vinafanana na magereza.
Friday, 28 October 2016
Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 29/10/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (BLM), Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein,
kesho tarehe 29/10/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati Maalum
ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa leo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar –
Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Waride Bakar Jabu, amesema kikao hicho
cha kawaida cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui
kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Amesema kikao pamoja na mambo
mengine, kitapokea na kujadili taarifa mbali mbali kutoka Idara na
Vitengo vya Chama hicho na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Aidha, Katibu Waride amesema kikao
hicho kilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,
kilichokutana tarehe 26 Octoba, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, kwa lengo la
kuandaa Agenda za kikao hicho.
“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”
Waride Bakar Jabu
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Itikadi na Uenezi – CCM
ZANZIBAR.
28/10/2016
Uzinduzi wa Ligi ya Taifa ya Wanawake unatarajiwa kufanyika Novemba 1 2016
Uzinduzi wa
Ligi ya Taifa ya Wanawake unatarajiwa kufanyika Novemba 1, 2016 kwenye
Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika mchezo ambao Baobao itacheza na
Victoria Queens ya Kagera.
Ligi hiyo ya kwanza kufanyika
nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati
imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv ambao wamedhamini kwa
kuonyesha mubashari (live), michezo hiyo 30 itakayofanyika viwanja
mbalimbali.
TFF imepeleka uzinduzi huo Dodoma
ikiwa na lengo la kuhamasisha soka mikoani tofauti na Dar es Salaam
ambako ilizoeleka zaidi miaka ya nyuma kabla ya kuwa na mpango wa
mashindano ya aina hiyo yanayoshirikisha timu 12 kutoka kona mbalimbali
za nchi.
Kadhalika, kwa siku ya Novemba
mosi ya uzinduzi huo vingozi wengi wa Serikali wakiwamo wabunge
wanatajiwa kuwa Dodoma ambako watapata fursa pekee ya kushuhudia
burudani ya mpira wa miguu wa ushindani itakayosukuma hamasa ya kutoa
michango yao mbalimbali kwa ajili ya soka la wanawake.
Mbali ya mchezo huo wa kundi B
kati ya Baobao na Victoria, michezo mingine itakuwa ni kati ya Sisterz
na Panama utakaofanyika Uwanja wa Tanganyika huko Kigoma wakati Marsh
Academy ya Mwanza itacheza na Majengo Women ya Singida kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kundi A kutakuwa na michezo mitatu
ambako Viva Queens ya Mtwara itacheza na Mburahati Queens ya Dar es
Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Fair Play ya Tanga
itapambana na Evergreen ya Dar Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja
wa Mkwakwani mjini Tanga huku JKT Queens ikiwa ni wenyeji wa Mlandizi
Queens ya Pwani kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Habari Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba na Sheikh
Shabaan Kitila baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini
Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam baada ya Sala ya
Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya waumini wa dini ya
Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza baada ya sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini
Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa Tanzania
wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri akiwa
katika Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma
Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Subscribe to:
Posts (Atom)