Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jijini Dar es salaam wakati alipotangaza jina la mgeni rasmi wa
Tamasha la Pasaka mwaka huu litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza ambaye ni Mh. Nape Nnauye Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo , amesema Mh. Nape Nnauye amelipa heshima tamasha la
pasaka na amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo jijini Mwanza,
Msama amemshukuru Waziri Nape kwa kumtambua mungu na kushiriki katika
kazi hiyo ya Mungu siku ya tarehe 27 mwezi Machi mwaka huu.
Akiongelea waimbaji ambao tayari
wamethiitisha kushiriki katika tamasha hilo amewataba baadhi kuwa ni
Upendo Nkone, Faustine Munishi, Ephraim Sekereti kutoka Zambia, Rose
Muhando Jesca BM , Bony Mwaiteje na wengine wengi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari
wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es
salaam.
Wakuu wa Mikoa wapewa jukumu la kutoa vibali vya kuchangia Elimu
Serikali imeongeza wigo wa utoaji
wa kibali cha uchangiaji wa elimu msingi bila malipo hadi kwa Wakuu wa
Mikoa baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zilizowekwa zimefuatwa
kikamilifu.
Katika taarifa yake kwa vyombo
vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema
kuwa awali vibali hivyo vilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pekee ikiwa na lengo la
kudhibiti michango holela.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa
azma ya Serikali ya kutoa elimu msingi bila malipo haizuii wadau
mbalimbali wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ambapo wadau
wakiamua kuchangia kwa nia ya kushughulikia kero fulani iliyopo katika
shule yao au shule zao baada ya kupata kibali wanaruhusiwa kufanya
hivyo.
Katika kutekeleza dhana ya utoaji
wa elimumsingi bila malipo, hadi kufika mwishoni mwa mwezi Januari,
2016 Serikali inatoa elimu hiyo kwa jumla ya wanafunzi 9,771,902.
Kati ya wanafunzi hao, 8,301,759
ni wa elimu ya msingi na 1,470,143 ni wa sekondari ambao wanapatiwa
elimumsingi bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Serikali inasisistiza kuwa
viongozi wanahusika katika kusimamia utekelezaji wake ambapo kwa upande
wa wazazi au walezi, kamati na Bodi ya shule pamoja na jamii wao nao
wanajukumu la kuelewa majukumu yao ipasavyo.
Aidha, juhudi za makusudi
zinapaswa kufanywa na viongozi na watendaji wa elimu ili kuwezesha jamii
kufahamu wajibu wao katika utekelezaji wa elimumsingi bila malipo na
hatimaye kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Katika kutekeleza wajibu wake,
Serikali ya Awamu ya Tano (SAT) kuanzia mwezi Januari, mwaka huu imeanza
kutoa elimumsingi bila malipo imetoa waraka wa Elimu Namba 6 wa Mwaka
2015 ambao unaofafanua na kubainisha majukumu ya serikali na wadau
mbalimbali katika utekelezaji wa elimu msingi bila malipo.
No comments:
Post a Comment