Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao
kesho Jumanne, wapenzi Wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za
kushuhudia mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es
salaam.
TFF inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata tiketi za mchezo huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika vituo walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha zao.
Zoezi la kuwarudishia fedha
washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za mchezo kati ya Tanzania v Chad
litafanyika katika vituo vinne vilivyokua vikiuza tiketi siku ya
Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo wanaombwa kufika na tiketi
zao ili waweza kurudishiwa fedha zao.
Aidha TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu uliojitokeza Na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Wanasubiria Taarifa zaidi kutoka CAF.
Chad imejiondoa jana katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017, ambapo iliku kundi G na timu za Misri, Nigeria Pamoja na Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu Wa MamlakaYa Usafiri Wa Anga Kuwait Mhandisi Yousef Al Fozan Awasili Nchini Kusaini Makubaliano Ya Usafiri Wa Anga Na TCAA.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan ,
maoja na Msafara wake Wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari,
(wapili kushoto) akiwa na maofisa wa Ubalozi wa Kuwait hapa nchini
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar
es alaam wakimsubiria Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan aliyewasili nchini kwa ajili ya kusaini
makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari
(Kushoto)akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan ,mara baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
leo,Kwa ajili ya kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya
Tanzania na Kuwait.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari,
(wapili kushoto) akiwa kwenye gari pamoja na wageni wake kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al
Fozan na Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Ubalozi Wa Kuwait Nchini, Mohamed
Rashid Alamiri, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege Wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo,Kwa ajili ya
kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari,
(wapili kushoto) akiwa na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan, wakati alipowasili
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar
es alaam kwa ajili ya kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya
Tanzania na Kuwait.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef
Al Fozan ,(Kulia) Akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari, kuhusiana na usafiri wa
Anga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo,Kwa ajili ya kusaini
makubaliano ya Safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
No comments:
Post a Comment