Wednesday, 23 March 2016

Waziri Ummy azungumza na Viongozi na Baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Dar leo

MWL1
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) Akizungumza na wazee wa mkoa wa Dare s Salaam walipokutana katika kikao ofisini kwake Leo (Katikati) ni Mwenyekiti wa baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali na kulia ni katibu wa wazee hao  Mohamed Mtulia.
MWL2
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).
MWL3
Katibu wa  wazee wa Dar es Salaam Mohamed Mtulia (Kulia) akizungumza wakati wa kikao  na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu (kushoto) na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali.
MWL4
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(Kulia) Akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
MWL5
Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi akizungumza katika kikao kilichojumuisha baadhi ya wazee wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
MWL6
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Dar es Salaam Bi. Mary Chipungahelo(maarufu kama mama Chips) Akichangia mada katika kikao kati ya baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
MWL7
Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
MWL8
Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
MWL9
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wazee wa mkoa wa Dar es salaam kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga na kulia ni Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi.


Na Tabu Mullah

Serikali imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.

Waziri Ummy amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku Nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao Muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya Wazee nchini na kuipeleka katika Bungeni mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.

Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.

Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini Yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni Bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.

No comments:

Post a Comment