Kundi la Haki za
kibinadamu Amnesty International limeishtumu Qatar kwa kuwafanyisha watu
kazi kwa lazima katika uwanja utakaochezewa Mechi ya Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022.

Uwanja wa Kombe la dunia nchini Qatar
Pia imelishtumu Shirikisho la soka Duniani Fifa kwa kushindwa kuzuia Dimba hilo linaloandaliwa Chini ya Unyanyasaji wa haki za kibinadamu.
Qatar imesema kuwa ina wasiwasi kuhusu madai hayo na kwamba itayachunguza.
Serikali ilisema kuwa maslahi ya wafanyikazi wahamiaji yanapewa kipaumbele na kusisitiza kuhusu Marekebisho ya sheria za kazi nchini humo.

Lakini Amnesti imeonya kwamba marekebisho hayo Hayataleta Tofauti yoyote na kusema kwamba Baadhi Ya Wafanyakazi ''Wanakabiliwa na wakati mgumu''.
No comments:
Post a Comment