Uongozi wa kampuni ya Kikundi cha
Waadhirika wa Maendeleo (KICHAWA) unaojishughulisha na Usafirishaji wa
mizigo wamezindua mwongozo wa mfumo shirikishi wa uratibu wa Bodaboda
na Bajaji nchini.
Akizindua mfumo huo leo Jijini Dar
es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mussa Chengulla na kusema
kuwa lengo ni kupambana na kupata suluhiso la kudumu katika sekta ya Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji juu ya changamoto za kisheria,
kiusalama na
kimazingira.Chengulla amesema kuwa sababu zilizopelekea
kuanzishwa kwa mfumo huo ni Matokeo makubwa ya changamoto zilizojitokeza
katika jamii juu ya wizi wa pikipiki, wizi wa kutumia pikipiki,
uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, kanuni za usafirishaji,
matumizi ya Kujichukulia sheria mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na
bajaji na ukamataji usio salama.
“Uwanzishwaji wa mfumo huu
shirikishi ni kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya
Usafirishaji na kutatua kero hatarishi zinazoikabili jamii ili kufika
malengo ya kuiondoa ajira ya Bodaboda na bajaji katika orodha ya ajira
hatarishi, kero na janga la Taifa na kuifanya kuwa ajira Tegemezi,
endelevu na salama kwa usalama wa raia na mali zao” aliongeza Bw.
Chengulla.
Mbali na hayo Bw. Chengulla
amesema kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi ni TAMISEMI Halmashauri
ya Manispaa ya Wilaya kwa kutambua idadi kamili ya wanaoendelea
kujiajiri na kuajiriwa kupitia sekta ya Usafirishaji abiria.
Pia Wengine watakaonufaika na
mfumo huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Jeshi
la Polisi na Usalama ya Raia na kitengo cha usalama barabarani, wamiliki
na Madereva wa bodaboda na bajaji kulingana na kazi za sekta husika.
No comments:
Post a Comment