Tuesday, 22 March 2016

Ukawa Washinda Umeya wa Jiji la Dar es Salaam Wamepata Kura 84, CCM Kura 67

 
Na Tabu Mullah

Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam Umekamilika leo katika Ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa Mshindi wa uchaguzi huo.

Mwita ameibuka na Ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam Baada ya kupata kura 84 akimshinda Mpinzani wake, Yenga Omary  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 67.

Uchaguzi huo Umeweka Historia ambapo kwa Mara ya kwanza Tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa vyama vingi (1992), Chama Cha Upinzani kimepata nafasi ya kuongoza Jiji Hilo.

Uchaguzi huo Uliahirishwa mara kadhaa kutokana na mvutano uliokuwa unaibuka kati ya Wajumbe wa CCM na Chadema na kuzua Vurugu Wakati mwingine.

Tofauti na ilivyo kwa Tarehe Nyingine za uchaguzi Zilizopangwa na kuahirishwa Wakati Wajumbe wakiwa Ukumbini, Viongozi wa Ngazi za Juu wa Chadema pamoja Na Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa Walihudhuria kushuhudia Uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment