Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) bw. David Mziray akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini
Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi Yaliyobainika kukiuka masharti
ya Leseni nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank
Mvungi.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari
uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta
hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo.
Kalonga Kasati
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,Kikosi
cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es
salaam,ambapo Wamefanikiwa kukamata mabasi 105 na kati hayo 36
yamefikishwa mahakamani baada ya kukiuka wa masharti ya leseni ya
usafirishaji abiria.
Hayo yamwebainishwa leo na Meneja
Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray wakati wa Mkutano na vyombo vya
habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na
Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za
asubuhi na Jioni.
Akifafanua Mziray amesema kati ya
Machi 21-24 , 2016 ilifanya ukaguzi huo na ili sheria iweze kuchukua
mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.
“Katika kuimarisha huduma za
usafiri Mamlaka imeweka utaratibu maalum wa kufanya ukaguzi katika
maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo katikati ya
jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale wote wanaovunja
sheria”.alisisistiza Mziray.
Akizungumzia baadhi ya makosa
yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema kuwa ni Pamoja na
kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya
usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.
Wamiliki na wafanyakazi katika
sekta ya usafirishaji kote nchini hasa wa mabasi ya daladala Wametakiwa
kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wanapotoa huduma hiyo kwa
umma.
Mziray aliongeza kwamba wananchi
wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale Wanapobaini basi
walilopanda linakiuka masharti ya leseni ikiwemo kuongeza nauli,kukata Njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji na kutoa huduma katika
njia ambazo hawakupangiwa Ambapo wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia
namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020.
No comments:
Post a Comment