Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally
Ungando akiwaonyesha wananchi cheti maalumu cha pongezi alichopatiwa na
Chama cha walemavu kwa ajili mchango wake mkubwa katika kuisaidia jamii
kushoto kwake ni Katibu wa chama cha waemavu Kibati Selemani
Zalala,
Na Chrispino Mpinge
MBUNGE wa Jimbo la Kibiti Ally
Ungando amewataka watendaji na viongozi kutokuwa wazembe Na kuachana
na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawajibike ipasavyo
kuwatumikia wananachi wao ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika
kukuza maenedeleo.
Kauli hiyo ameitoa katika
mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bungu ulioandaliwa kwa lengo
la kuweza kuwashukuru kwa kuweza kumpatia nafasi ya kuwaongoza kwa
kipindi cha Miaka mitano ambapo ulihuiwa wa na viongozi wa serikali
pamoja na watendaji wa kijiji,kata pamoja na Wilaya.
Ungando alisema kwamba
serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuleta mabadiliko hivyo
kwa upande wake hawezi kuwavumilia wale wote ambao watabainika wanafanya
kazi kwa kuangalia maslahi yao binafsi bila kuangalia vipaumbele
wanavyovihitaji wananchi hao.
Aidha Mbunge huyo amebainisha
kwamba baadhi huduma za kijamii ambazo zilikuwa zimekwama ikiwemo
afya,elimu,vyoo pamoja na mambo mengine kutokana na kuwepo kwa
utendaji mbovu ameahidi kuzitatua haraka iwezekanavyo iii wananchi
waweze kuondokana na kero hizo.
Pia Mbunge huyo wa Jimbo la
Kibiti ameahidi kutoa mabati 100 kufanikisha ujenzi wa shule ya msingi
Kibwibwi kuwawezesha wanafunzi kupata huduma ya elimu karibu na
wanapoishi.
Ungando alisema, bati hizo
zitatokana na fedha za mfuko wa jimbo, lengo likiwa ni kutatua
changamoto zinazokwamisha maendeleo katika jimbo hilo.
Aidha aliwaomba wananchi
kudumisha ushirikiano kufanikisha kuleta mabadiliko ya kimaendeleo
katika jimbo la kibiti ikiwemo kuepusha migongano ambayo inadumaza
maendeleo.
Kwa upande wake Afisa mtendaji
wa kata ya Bungu Mohamed Mketo alisema asilimia kubwa ya Watoto
wanaoishi katika kitongoji cha Kibwibwi wanashindwa kuendelea na masomo
kutokana na umbali mrefu.
Nao baadhi ya wananchi
waliofika katika mkutano huo hawakusita kutoa kilio chao
kinachowakabili akiwemo Salum Kasuku,Salum Pazi,pamoja na Asia Mohamed
walisema Wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo huduma ya afya,
ukosefu wa maji safi na salama pamoja na kukabiliwa na uhaba wa
wauguzi pamoja na madaktari.
Kwa upande wake Diwani wa kata
ya bungu Ramadhani Mpendu akijibu baadhi ya malalamiko Yaliyotolewa na
wananchi hao katika mkutano huo amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na
kuahidi kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
No comments:
Post a Comment