Na Tabu Mullah
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Ilala wamepewa mpaka tarehe 24 Marchi mwaka huu Wawe wamekwenda
kuhakikiwa katika ofisi za utawala za Halmashauri hiyo katika kutekeleza Agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuhakiki watumishi wote wa
umma.
Akizungumza kwa njia ya simu
ofisini kwake msemaji wa Halmashauri ya Ilala Bi. Tabu Shahibu Amesema
tangazo limeshatoka na watumishi wote wanatakiwa kufika kuhakikiwa
katika ofisi za Utawala ambapo wanatakiwa kwenda na nyaraka mbalimbali
muhimu zizohusu ajira zao.
Bi Tabu Shahibu amezitaja nyaraka
hizo ambazo mtumishi anatakiwa kuambatanisha wakati wa Uhakiki wake kuwa
ni vyeti halisi vya taaluma,barua ya kuajiriwa na kudhibitishwa kazini,
salary slip na picha ndogo za hivi karibuni.
“Zoezi la Uhakiki linaendelea
vizuri na watumishi wengi wamejitokeza kwa wingi na tunategemea kumaliza
zoezi hili March 24 mwaka huu ili kuandaa taarifa rasmi ya kujua
watumishi halali na wale watumishi hewa” Alisema Bi Tabu.
Aidha Bi Tabu Shaibu amesema
kumekuwa na changamoto ya watumishi wengi kutokuwepo kwenye vituo vya
kazi ikiwa wengine wapo masomoni na likizo ila wameshatoa taarifa ya
kuwaita ili kufanyiwa uhakiki mara moja ili kuendana na muda uliotolewa
na Mhe Rais Magufuli wa siku 15.
Zoezi la uhakiki wa watumishi wa
umma katika limekuja mara baada ya uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya
Singida na Dodoma katika Halmashauri 14 na kugunduwa wafanyakazi hewa
202 Wanaolipwa mishahara na hivyo Mhe. Rais Magufuli kutoa agizo la
kuhakiki watumishi wote Katika Wizara,mikoa,Wilaya,Idara,Taasisi na
Wakala za Serikali ndani ya siku 15.
No comments:
Post a Comment