Afisa
Usalama wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Henry
Byarugaba akionyesha Moja ya eneo ambalo wameiba umeme kwa
kujiunganishia bila ya kuzingatia taratibu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo wakiwa katika eneo hilo mara baada ya kubaini kuwepo kwa wizi huo wa umeme.
Na Mwamvita Mtanda
SHIRIKA la ugavi wa umeme
Tanesco Mkoani Pwani limewakamata watu saba kwa tuhuma za Wizi wa
umeme katika eneo la kwamfipa Wilayani Kibaha ambao walikuwa
wamehujumu Miundombinu kwa kujiunganishia umeme kinyemela kinyume cha
utaratibu.
Akizungumzia kuhusina na tukio
hilo Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Herny Byarugaba amesema
kwamba kubainika kwa watu hao waliokuwa wanaiba umeme kumetokana baada
ya kupatiwa taarifa kutoka kwa wananchi wasamalia wema wa eneo hilo.
Byarugaba amesema kwamba wezi
hao walikuwa wamezichimbia nyaya za umeme chini ya Barabara ya
kuusambaza katika baadhi ya maeneo ikiwemo maduka, mabanda ya
kuonenyeshea video hali ambao amedai ni hatari kwa usalama wa maisha ya
watu kwani kunaweza kutokea Majanga ya kuungua kwa nyuma za watu na
kupoteza maisha yao.
“Sisi tumepata taarifa hizi
kutoka kwa wananchi wasamalia wema kwa hiyo sisi kama tanesco Tukaamua
kufanya msako mkali katika eneo hili la kwa mfipa na kuweza kukuta
wateja wetu Wameamua kutumia njia za kinyemela kwa kuiba umeme na mbaya
zaidi nyaya wamezipitishia Chini kabisa ya barabara hivyo hali hii ni
hatari sana watu wanaweza kupoteza maisha,”alisem Byarugaba.
Aidha alibainisha kwamba
kutokana na kujiunganishia umeme kinyume na taratibu kunaweza kuleta
madhara makubwa kwa wananchi kwani pindi mvua inaponyesha na nyaya hizo
zikiwa Zimechunika maji yanashika umeme na hivyo kunaweza kusababisha
hatari kubwa sana.
Pia Byarugaba aliongeza kuwa
Shirika la Tanesco limekuwa linapata hasara kubwa na kupoteza mapato
yake kutokana na baadhi ya watu kuamua kufanya vitendo vya hatari vya
kuhujumu miundombinu yao pamoja na kuiba umeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
serikali ya mtaa kwamfipa Juma Tanga ambaye alifika eneo la Tukio
alisema kwamba amesikitishwa sana kuona baadhi ya wananchi wake
kushiriki kuiba Umeme kinyume na taratibu na kuwataka waachane na
vitendo hivyo kwani ni hatari kwa usalama wa maisha yao.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba
katika kukabiliana na hali hiyo atahakikisha anaweka Mikakati ya
kuwaelimisha wananchi wake katika mikutano mbali mbali kuhusina na
madhara Ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na kujiunganishai umeme bila
ya kuzingatia taratibu zilizowekwa na wahusika wenyewe.
Naye Meneje wa Tanesco Mkoa wa
Pwani Martin Madulu ametoa tahadhari kwa wananchi wote Wa Mkoa wa
Pwani kuachana kabisa na tabia ya kujiunganishia umeme pasipo kuwatumia Wafanyakazi husika wa tanesco na badala wake wahakikishe wazingatie
taratibu katika kuunganishiwa umeme katika sehemu za biashara pamoja na
nyuma za kuishi.
Aidha katika hatua nyingine
Mejeja huyo aliwataka wananchi kujihadhari ya matapeli ambao Wanajifanya
ni wafanyakazi wa shirika hilo na endapo wakiwabaini watoe taarifa
mapema katika Vyombo vinavyohusika ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
No comments:
Post a Comment