Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)
inatarajiwa kucheza michezo miwili Ya kirafiki na timu ya Taifa ya Misri
Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (The Pharaohs) jijini Dar es
salaam.
Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti
Boys dhidi ya The Pharaohs utachezwa siku ya Jumamosi, Aprili 2 katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa pili ukichezwa
Jumanne Aprili 5 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Msafara wa The Pharaohs
unatarajiwa kuwasili Alhamis tarehe 31, Machi ukiwa na watu 33, Wakiwemo
wachezaji 25 pamoja na viongozi 8, na wataondoka nchini tarehe 6 Aprili
kurudi kwao nchini Misri.
Kikosi cha Serengeti Boys
kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa Wakishauriwa
na Jan Poulsen, kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume, zilipo
ofisi za Makao za Makuu ya TFF.
Serengeti Boys ilingia kambini
takribani wiki mbili zilizopita katika hosteli za TFF zilizopo Karume,
kujiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri
chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.
Tanzania itaanza kuwania kufuzu
kwa fainali hizo mwishoni mwa mwezi Juni, kwa kucheza dhidi ya Timu ya
Taifa ya Vijana ya Shelisheli.
No comments:
Post a Comment