RC DAR ES SALAAM APIGA MARUFUKU UTOAJI WA VIBALI VYA MALORI YA MIZIGO YENYE UZITO WA ZAIDI YA TANI 10 KUINGIA KATIKATI YA JIJI.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Saidi Mecki Sadiki akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa
Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kwa mwaka 2016.
Kulia ni Zungu Azzan na Kushoto ni Bw. Edward Otieno Kaimu Katibu Tawala
wa mkoa huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Bw.Isaya Mngurumi akichangia jambo kuhusu uboreshaji wa Miundombinu ya
barabara katika Manispaa yake wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya
Barabara Mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia
Mjema akichangia jambo wakati wa wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya
Barabara Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016.
Baadhi ya Wabunge wa jiji Dar es
salaam wakifuatilia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam.
Kutoka kulia ni Mhe. Bonnah Kalua – Mbunge wa Segerea, Mhe. Faustine
Ndugulile – Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Zungu Azzan – Mbunge wa Ilala na
Mhe. Abdallah Mtolea – Mbunge wa Temeke.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa
wa Dar es salaam Muhandisi Julius Ndyamkama akitoa ufafanuzi kwa
wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam kuhusu
miradi ya ujenzi wa Barabara inayosimamiwa na Wakala hiyo.
Na. Kalonga Kasati
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Saidi Mecki Sadiki amepiga marufuku utoaji wa vibali vya malori ya
mizigo na magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia katika barabara
zote zinazosimamiwa na Manispaa za jiji la Dar es salaam zilizojengwa
kwa kiwango cha lami kufuatia barabara hizo kuharibika kwa kipindi
kifupi kutokana uzito jambo linaloisababishia Serikali hasara.
Aidha, ameziagiza manispaa za
jiji hilo kuweka alama za barabarani zinaonyesha zuio kwa magari Yote
yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kupita kwenye barabara hizo ili wamiliki
na madereva watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka
2016 Mhe. Sadiki Meck Sadiki amesema kuwa Manispaa za jiji hilo
zinatenga Fedha nyingi za kujenga barabara mpya na kufanya matengenezo
ya zile zilizopo ambazo nyingi zinaharibiwa na malori ya mizigo.
Amefafanua kuwa Matumizi hayo Mabaya ya Barabara kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na Ukiukwaji wa sheria
za Barabarani ambapo Malori Makubwa ya Mizigo huegesha na kuziba maeneo Ya Waenda kwa Miguu Jambo linalowanyima haki Wananchi kutumia Maeneo Yaiyotengwa kwa ajili yao.
Amesema Baadhi ya Magari yenye Uzito wa tani 40 hudiriki kupita kwenye barabara za huduma (Service
road), Madaraja na wakati mwingine maeneo ya waenda kwa miguu jambo
linalosababisha Uvunjaji wa kingo za barabara na milingoti ya taa za
barabarani na kuongeza kuwa Vitendo hivyo Vinaisababishia Serikali Hasara kutokana na Gharama ya Matengenezo.
“Kuanzia leo katika Mkoa Wangu ni Marufuku kutoa vibali vya Magari yenye Uzito wa zaidi ya tani 10
kuingia kwenye barabara zetu, tunataka Barabara zetu zidumu, hatuwezi
kuvumilia vitendo vya Watu Wachache wanaokiuka Sheria za barabarani
kuharibu barabara zetu, lazima tuchukue hatua Manispaa zinajitahidi
kujenga Bararaba lakini hazidumu” Amesisitiza Mhe. Sadiki.
Amesema barabara zinazosimamiwa
na Manispaa za Dar es salaam zina uwezo wa kuhimili uzito Wa Tani 10 na
kubainisha kuwa kwa kipindi kirefu malori ya Tani 40 yamekuwa yakipita
kwenye Barabara hizo na kuzifanya manispaa kunajenga barabara hizo kila
mwaka.
Mhe. Sadiki amesema kuwa ipo haja
ya mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara katika jjiji la Dar
es salaam kwa kuwatumia wataalam wa sheria kuanza kuangalia uwezekano wa Wamiliki wa vyombo vinavyosababisha uharibifu wa miundombinu ya
barabara kulipa gharama za Uharibifu huo.
Kuhusu Ulinzi na Usalama
watumiaji wa barabara za jiji amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea
kuchukua Hatua na kufanya Operesheni dhidi ya madereva wa pikipiki
(Bodaboda) na Bajaji Wanaopitisha vyombo vyao vya Usafiri kwenye njia za Waenda kwa Miguu na kusababisha usumbufu na ajali za mara kwa mara kwa
wananchi wanaotumia njia hizo.
Pia amezitaka Manispaa za jiji
hilo kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es salaam
kusimamia maeneo yote yanayotakiwa kujengwa miundombinu ya Barabara ili Yasivamiwe na wananchi pamoja na kuwachukulia hatua wananchi wanaofanya
biashara katika Maeneo yasiyoruhusiwa ya hifadhi za barabara na njia za
waenda kwa miguu.
‘‘Ninaiagiza manispaa ya
Kinondoni kuondoa wafanyabishara wote walioko eneo la kituo cha
kuzalishia umeme Ubungo, eneo lile ni hatari kwa usalama na maisha yao,
kukaa pale ni kinyume cha sheria’’ Amesisitiza.
Aidha, amesema mwaka 2016 mkoa wa
Dar es salaam umetenga jumla ya Shilingi bilioni 343.5 ikilinganishwa
na Shilingi Biliobi 266.6 zilizotengwa mwaka 2015/2016 kutekeleza
ujenzi na Matengenezo ya Barabara katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo
lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari.
Kuhusu Kikao hicho cha kwanza cha
Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016 amesema pamoja
mambo mengine kimepokea na kujadili tarrifa utekelezwaji wa ujenzi wa Miradi ya barabara kwa mwaka 2015/2016 pamoja na kupokea Mpango wa
matengenezo ya barabara kwa mwaka 2016/2017.
Ametoa wito kwa wakazi wa jiji la
Dar es salaam kuzingatia usafi wa mazingira kwa kulinda Miundombinu ya Barabara na kuepuka kutupa taka kwenye mifereji ya kupitisha maji ili
kuzuia Mlipuko wa magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.
No comments:
Post a Comment