Thursday, 3 March 2016

Twiga Stars Tayari kuwavaa Zimbabwe kesho

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi Ya Mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika Mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa Mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo Asubuhi kwa kufanya Mazoezi Mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema Vijana wake Wote Wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye Mchezo huo.
Akiongea na waandishi wa Habari leo katika Ukumbi wa TFF uliopo Karume, Nasra amesema ana Waheshimu Zimbabwe wana Timu nzuri, ndani ya miaka Minne wameshacheza nao zaidi ya mara Nne, Mapungu yaliyojitokeza katika Michezo iliyopita Wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani watafanya vizuri.

Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Naye Nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, Wana ana ari na Morali ya Hali ya Juu kuelekea kwenye Mchezo Huo wa kesho, na kuwaomba Watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia Uwanjani Watakapokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania.

Wapinzani wa Twiga Stars, Timu ya Taifa ya Zimbabwe Wanawasili leo Jioni Tayari kwa mchezo huo, Huku waamuzi wa Mchezo huo kutoka nchini Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).

WANANCHI WACHOSHWA NA TAASISI YA VIZAZI NA VIFO (RITA) OFISI ZA PEMBA

download (13)
Na Mwamvita Hussein
 WANANCHI  wa Kisiwani Pemba wamesema kwamba wamechoshwa na vitendo nenda rudi nenda Rudi katika Ofisi za vizazi na vifo kufuatailia vyeti vya kuzaliwa na pamoja na vyeti vya vifo ambavyo upatikanaji wake unasumbua .

Wananchi hao  wamelalamika juu ya ucheleweshwaji wa vyeti hivyo   jambo ambalo limekuwa Nikikwazo kikubwa  katika upatikanaji  wa  haki  zao za msingi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamesema kuwa upatikanaji wa vyeti hivyo ni Tatizo la Muda Mrefu hali ambayo imesababisha baadhi wa watoto kuanza skuli bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa .
Aisha  Kombo Hassan Mkaazi wa Ukutini Mkoani alisema kwamba ufuatiliaji  wa vyeti katika Ofisi za Vizazi na Vifo za Wilaya , Mbali na Usumbufu anaoupata pia umekuwa ukiongeza Gharama anazotumia katika gari za abiria .

“Hata ukikipata cheti utakuwa imetumia zaidi ya Shilingi elfu ishirini , hii ni kutokana na Gharama Za kupanda katika Gari za abiria mara kwa mara kwa kweli Tunasumbuka sana ”alifahamisha .
Naye  Juma Ali Mohammed mkaazi wa Makangale , alisema kwamba wapo baadhi ya wananchi Wamekosa vitambulisho vya mzanzibar mkaazi kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa .

Alisema Wako Vijana ambao Wametmiza Umri wa kupiga kura , lakini wameshindwa kupata fursa Hiyo kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa ambavyo ndiyo vinavyopelekea kupata kitambulisho cha Mzanzibar .

Hali hiyo pia imelalamikiwa na Mwatime  Omar Issa Jojo Mchangamdogo ,  ambaye aliiomba  Serikali kuchukua hatua za makusudi kulipatia ufumbuzi suala hilo , ili wananchi wanaondokane na Usumbufu Wanaoupata kwa sasa .

 Kwa upande wake Mdhamini  Ofisi ya Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Mali Vizazi Na Vifo Pemba Salehe Mohd Abdalla amesema  hali hiyo inatokana na ufinyu wa bajeti katika Ofisi hiyo .
Alisema kuwa tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni kwani Ofisi hiyo inatagemea kupata Magamba elfu kumi (10000) kutoka Ofisi Kuu Unguja na watayagawanya kwa Ofisi za Wilaya  zote Pemba .

“Tunatarajia kupata Magamba elfu kumi , na yakifika tu tunayapeleka katika Ofisi za Vizazi za Wilaya , Naomba sana Wananchi wawe Wastahamilivu tatizo linafahamika ”alieleza.

Aidha alifahamisha kuwa kutokana na ongezeko la vizazi , Ofisi ya Pemba inahitaji kupata Magamba Angalau  Mia tatu (300) kila mwezi ili kukidhi haja na Mahitaji ya Wananchi .
Hata hivyo Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Habari hizi Umebaini kwamba Baadhi ya Wilaya kuna Wananchi Wanadai vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao kwa Zaidi ya Miaka Mitano sasa Bila ya Mafanikio .

No comments:

Post a Comment