Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa wodi ya Wazazi katika kijiji
cha Nyashimo wilaya ya Busega akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 2, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Busega, Dkt, Raphael Chegeni na
Kulia nI Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka watumishi na watendaji wote wa Serikali wahamie yalipo makao
makuu ya wilaya ya Busega kuanzia sasa ili kuleta kasi ya utendaji kazi
kwenye wilaya hiyo ambayo ni mpya.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumanne, Machi 2, 2016) wakati akizungumza na wananchi waliofika
kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la
Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara
ya siku sita ya mkoa huo atakagua shughuli za maendeleo na kusalimia na
wananchi katika wilaya zote za mkoa huo.
“Leo nimeagiza watumishi wote wa
umma katika wilaya hii wahame kutoka Magu ambako wanaishi hivi sasa na
wahamie hapa Busega ili wafanye kazi kutokea hapahapa. najua kuna
changamoto ya nyumba za watumishi lakini waje waishi kwenye nyumba za
kupanga wakati Serikali ikiendelea kushawishi NHC, NSSF na Mwananchi
Housing Corporation waje wajenge nyumba za watumishi kwenye halmashauri
mpya,” alisema.
Waziri Mkuu alisema kitendo cha
watumishi kuhamia yalipo makao makuu ya wilaya kitasaidia kuongeza kasi
ya kuleta maendeleo kwani watakuwa wanaziona changamoto zilizopo mahali
wanapoishi.
Alisema Serikali inao wajibu wa
kujenga ofisi na nyumba za watumishi na kuwahakikishia kuwa azma hiyo
itatimia kutokana na makusanyo ambayo Serikali imekuwa ikiyafanya hivi
sasa ikilinganisha na siku chache zilizopita.
Jengo hilo la Halmashauri
lililoanza kujengwa Julai 20, 2015 litagharimu sh. bilioni 4.66/- na
linatarajiwa kukamilika Januari 20, 2017.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa
mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Busega, Bibi Gaudensia
Bamugileki alisema changamoto kubwa inayowakabili ni kutopatiwa fedha
kwa wakati hali ambayo alisema kama itaendelea itaathiri ukamilishaji wa
jengo hilo kwa wakati.
“Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa
sh. milioni 600. Fedha ambazo zinahitajika kukamilisha ujenzi ni sh.
4,064,580,238/-. Tunaendelea kukumbushia fedha za ujenzi kutoka Serikali
kuu ili tupunguze gharama ya kodi inayolipwa kwa jengo la kukodi ambalo
pia halitoshelezi mahitaji ya vyumba vya ofisi kwa watendaji na
watumishi wa Halmashauri,” alisema.
Katika mkutano mwingine, mara
baada ya kukagua wodi ya akinamama, Waziri Mkuu alizungumza na wakazi wa
Nyashimo ambako wodi hiyo inajengwa na kuwahakikishia nia ya Serikali
kufikisha huduma bora kwa wananchi.
Alitoa shukrani kwa ubalozi wa
Japan kwa kuchangia ujenzi wa wodi kwa gharama ya dola za marekani
80,000 pamoja na nyongeza ya sh. milioni 312.1. Pia aliishukuru taasisi
ya Benjamin Mkapa Foundation ambayo tayari imejenga nyumba 10 za
watumishi kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Busega.
Pia alisisitiza elimu kwa watoto
wa kike na kumtaka Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Paul Mzindakaya afanye msako
wa kubaini wale wote ambao hawajaanza kidato cha kwanza hadi sasa.
“Serikali inataka watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wawe
wameripoti shuleni. DC wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya wilaya hii. Fuatilia na kuwachukulia hatua wote waaliozuia watoto
hawa wasiende shule,” alisema.
“Suala la ulinzi kwa watoto wa
kike hivi sasa ni la lazima. Ni lazima tuhakikishe mtoto akianza shule
ya awali anaingia darasa la kwanza lazima amalize darasa la saba.
Akiingia kidato cha kwanza, ni lazima amalize kidato cha nne, akiingia
kidato cha tano ni lazima amalize kidato cha sita,” alisisitiza huku
akishangiliwa.
Mapema, akitoa taarifa ya mkoa
huo, Mkuu wa Simiyu, Bw. Elaston aliomba kuongezewa ukomo wa bajeti ya
mkoa kwa mwaka kwa sababu mkoa huo ni mpya na una changamoto nyingi
ikilinganishwa na mikoa ya zamani ambayo haina mahitaji ya miundombinu.
“Mkoa wa Simiyu umetengewa ukomo
wa bajeti sh. 1,117,133,000.00 wakati mikoa ya zamani kama Morogoro
imetengewa sh. 2,836,225,000.00, Arusha (2,595,571,000.00), Kilimanjaro
(2,543,463,000.00) Mbeya (2,141,239,000.00) na Tanga (2,318,545,000.00).
Tunaomba tufikiriwa ili tuweze kuimarisha miundombinu ya ofisi,
barabara, na huduma za jamii katika mkoa huu,” alisema.
MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA, YAWAPIGA MSASA WANAHABARI KUHUSU EL-NINO NA ATHARI ZAKE.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana
Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Siku mbili kwa
Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini,
iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
…………………………………………………………………………………
Katika
Warsha hiyo, Taasisi mbalimbali pamoja na Wanajamii, zimehimizwa
kutumia taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa kwa ajili ya Mipango ya
Maendeleo.
Pia
Wanahabari ambao ni kiunganishi Muhimu katika upashanaji wa habari,
wametakiwa kutumia nafasi yao katika kutoa taarifa hizo kwa wananchi
ikizingatiwa kwamba, taarifa za utabiri wa hali ya hewa zikiwafikia
walengwa kwa wakati, husaidia kujikinga na maafa yatokanayo na
mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Mafuriko na ukame.
Warsha
hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kwa
ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) ikiwa ni
katika mpango wake wa Kidunia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa za
hali ya hewa ujulikanao kama Global Framework For Climate Services
(GFCS).
Katibu
Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa
nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Ziwa, Augustino Nduganda akitoa neno la Shukrani baada ya Ufunguzi wa Semna kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini.
Wengine
kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa
nchini, Hamza Kabelwa, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Marcella Mayalla, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
Alphonce Tonny kutoka Metro Fm Mwanza (Kushoto) akiwa pamoja na Iman Hezron Kutoka City Fm Mwanza.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
No comments:
Post a Comment