Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu
ya matumizi ya jiko linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa
Tanzania Agriculture Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika
ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi
Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (mwenye koti la Draft) akitoa
ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring wa Sinza Dar es
Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali yaliyofanyika Jijini Dar
es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther
Riwa.
Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya
Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki (Hawapo pichani) wa mafunzo
ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya vijana wakimsikiliza
mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo cha kisasa kwa vijna
katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na kushirikisha vijana
toka Dar es salaam na pwani.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya
kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John akitoa neno la Shukrani kwa
mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku
tatu Jijini Dar es salaam.
Na Tabu Mullah
Katika kuboresha na kuongeza
ajira hapa nchini Serikali imeahidi kuwapatia Vijana mtaji na Maeneo
kwa ajili ya kilimo cha kisasa ili waweze kujiendeleza na kukuza
kipato chao.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha “Green Houses”
Mkurugenzi Wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu,
Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na watu Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi
amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa mbalimbali
zinazojitokeza katika kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.
Ameongeza kuwa Serikali
inaendelea kuwawezesha kupata mikopo kwa riba nafuu na kutoa elimu
kuhusu kilimo bora cha kisasa ili kuondoa fikra zilizopo kwa vijana
kuwa kilimo ni kwa ajili ya Watu waliokosa Elimu,wenye Maisha duni na
wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Ni lazima tutumie fursa Zinazojitokeza katika kunufaika,nina imani mtatumia fursa hii kwa Manufaa yenu na Elimu Mtakayopata itawasaidia kuzalisha bidhaa bora na
kuondoa utegemezi. Alisema Mkurugenzi Kajugusi”.
Aidha mwezeshaji wa mafunzo hayo
Bw Praygod Mushi amewataka vijana hao kuamini kuwa kilimo kinaweza
kubadilisha maisha yao kama watatumia fursa zote zinazojitokeza katika
sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.
Naye mmoja wa washiriki katika
mafunzo hayo Bi Jasmini John ameishukuru Serikali kwa kuaandaa mafunzo
hayo na kusema kuwa atatumia elimu atakayopata kuendeleza kilimo kama
ajira kwa kutumia pembejeo za kisasa atakazoelekezwa katika mafunzo
hayo.
Mafunzo ambayo vijana hao
wamepewa ni Jinsi ya kutumia dawa na mbegu bora katika
kilimo,kunufaika na mazao yatokanayo na kilimo cha Green House,utunzaji
wa mazingira kwa kutumia Nishati ya mwanga wa jua pamoja na ubunifu wa
shughuli za vijana katika jitihada za kukuza viwanda kwa kutumia mali
ghafi za humu nchini.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu kuanzia leo na yameshirikisha vijana kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
No comments:
Post a Comment