Thursday, 3 March 2016

Wasambazaji wa Filamu Tanzania Waipongeza Serikali

mwa1
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifamba (Kushoto) akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati akitoa pongezi za Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa Serikali ya Awamu ya Tano katika mkutano na waandishi wa habari.

Na Tabu Mullah
Chama cha Wasambazaji wa Filamu Tanzania kimeipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa juhudi Zake inazozifanya katika kupambana na uharamia kwenye sekta ya filamu Tanzania.
Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifamba alipokuwa Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kuunga mkono juhudi madhubuti Za Serikali za kudhibiti uharamia wa kazi za filamu haswa kwenye eneo la mauzo la sokoni Kariakoo.
“Kwa takribani miaka mitatu sasa tumekuwa na kilio cha wazi kwa Serikaliya Tanzania iliitusaidie kuwabana wahujumu wa mapato ya nchi unaofanyika kupitia njia za kiharamia zinazotumika kuuza kazi za filamu Ndani na nje ya Nchi.

Kilio Chetu kimesikilizwa natunaamini tija ya soko la filamu litaanza kuonekana ndani ya Muda Mfupi kuanzia sasa.”AlisemaMwakifamba.

Pia,ametoa Rai kwa Serikali kutolegeza kamba bali kuzidi kulidumisha zoezi hili la kudhibiti Mianya Yote ya Uharamia ili wasambazaji watumie utaratibu unaotakiwa na Serikali katika Usambazaji wa kazi za filamu.
Kwa kipindi kirefu sasa wasanii nchini wamekuwa wakipambana na unyonywaji wa kazi zao za filamu Unaofanywa na wasambazaji wa filamu wasio halali ambao wanapunguza mapato ya wasanii Na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment