Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akisalimiana na
Mkurugenzi mkuu National Media Group Bw.Joe Muganda wakati wa tafrija
fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications limited kwa
ajili ya Bodi ya Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiwasili katika
hoteli ya Serena kwa ajili ya tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya
Mwananchi Communications limited kwa ajili ya Bodi ya Mwananchi,wateja
wake na wadau wa Habari.
Mkurugenzi Idara ya Habari
Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akifurahia jambo na Mhariri Mtendaji
wa Magazeti ya Mwananchi Communications Limited Bakari Machumu wakati
wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya hiyo kwa ajili ya Bodi ya
Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akizungumza na wadau
wa Habari wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi
Communications Limited.Mheshimiwa wambura alivishukuru vyombo vya habari
kwa kuhabarisha watanzania kipindi cha uchaguzi na pia katika siku mia
za kwanza za Rais wa awamu ya tano na Mhe.John Pombe Magufuli na
kuwapongeza kwa kuonyesha weledi na ukomavu katika uandishi wa Habari.
Wadau wa Habari wakifatilia
hotuba ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura.Kutoka kushoto ni Bi.Teddy Mapunda na Mwisho kulia ni Maria
Sarungi
Afisa Mtendaji mkuu wa Star Times
Tanzania Bw.Leo Liofang(wa kwanza Kulia) pamoja na Makamu wa Rais wa
kampuni ya Star Times Bi. Zuhura Hanif(wa pili Kulia) wakifatilia jambo Wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi
Communications limited kwa ajili ya Bodi ya Mwananchi,wateja wake na
wadau wa Habari.
Na Kalonga Kasati
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura Amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kuwahabarisha Watanzania vyema katika
mchakato wote Wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na katika kipindi cha siku
mia za kwanza za awamu ya tano ya utawala wa Mheshimiwa Dr. John Joseph
Pombe Magufuli.
Naibu Waziri uyo ameyasema hayo
alipokuwa akiongea na wadau wa Habari katika tafrija fupi iliyoandaliwa
na kampuni ya Mwananchi Communications Limited.
“Hakika mmeonesha uwezo mkubwa, weledi na ukomavu mkubwa wa kisiasa na uzalendo kwa nchi yetu”.Alisema Bi.Wambura.
Mhe.Wambura pia alieleza kuwa
Serikali ya awamu ya Tano ina Dhamira ya Dhati kabisa ya Kushirikiana na Wadau wote Vikiwemo Vyombo vya Habari, ambapo pia Mchakato wa Sheria ya
Huduma za Vyombo vya Habari ambao Ulishasomwa kwa Mara ya kwanza
bungeni bado Serikali inaendelea kupokea Maoni ya wadau mbalimbali juu
ya namna Bora ya kuboresha Muswada huo.
Naibu Waziri Uyo alikazia Umuhimu
wa Upashaji habari na kusema ni Jambo Muhimu sana katika Nchi yetu na
kwaiyo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo iko Tayari kufanya
kazi na Wadau wote.
“Kama Serikali hatuwezi kuwakwepa Wadau na ndio Maana hata Utaratibu wetu wa kushughulikia Makosa kwenye
Vyombo vya Habari umebadilika. Tumekuwa ni walezi zaidi badala ya kuwa Viranja. Tunashauriana Zaidi kuliko kutoa Adhabu. Tunaelimisha zaidi
kuliko kusubiliana”
Naibu Waziri uyo pia aliupongeza Uongozi mpya wa jukwaa la wahariri na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa
karibu katika kutatua Masuala mbalimbali ya Habari.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti
Mtendaji wa Bodi ya Magazeti ya Mwananchi Bw.Francis Nanai Aliipongeza Serikali kwa kuweka jitihada zaidi katika kuboresha Mahusiano Mazuri na
vyombo vya Habari na pia kwa Afrika Mashariki Tanzania iko katika Nafasi
nzuri Ukilinganisha na Wenzetu katika suala la Uhuru wa vyombo vya
habari.
No comments:
Post a Comment