Monday, 7 March 2016

Vaeni Joho La Uadilifu-Angela Kairuki

images (14)
 
 
Na Kalonga Kasati

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora mhe. Angellah Kairuki amewataka wenza Wa viongozi wa Umma nchini kuvaa joho la uadilifu ili kuiletea maendeleo ya kweli nchi
Mhe. Kairuki ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam Wakati akifungua Mafunzo ya Maadili kwa Wenza wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.
 
‘Niwaombe washiriki wa Mafunzo haya, Mvae joho la uadilifu na kwa wale Wanaoendana na Mienendo hii ya Maadili niwasihi Muishi na kuendelea kuishi katika Maadili hayo’.
 
Amesema Wenza hao wakiishi kwa kufuata uadilifu unavyotaka Harakati za kuwa na Tanzania ya Waadilifu zitashamiri na hivyo kuiletea nchi Maendeleo Makubwa.
 
Amesema Usimamizi wa Maadili sio wa Serikali pekee Jambo hili linapaswa kuwa Jukumu la kila Mmoja wetu.
 
‘Usimamizi wa Maadili sio wa Serikali pekee, hili linapaswa kuwa Jukumu letu Sote kama Taifa’, Alisema Mhe. Kairuki na kuongeza kuwa Maadili ni Wajibu Wetu sote, Tushirikiane ili tuweze kulikabili suala la Mmomonyoko wa Maadili ambalo linaikabili nchi hii’. 
 
Aidha Mhe. Kairuki aliwataka wenza hao wa viongozi kuhakikisha Yanakuwepo Matumizi Sahihi Za Rasilimali za Taifa ambazo wenza wao wamekabidhiwa kwa ajili ya Matumizi yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment