Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi John William Kijazi.
Na Tabu Mullah
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Katibu Mkuu
Kiongozi mpya Balozi John William Kijazi.
Sherehe hizo za kuapishwa Zimefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia uteuzi uliyofanyika Jana baada ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kumaliza muda
wake.
Naye Katibu Mkuu Kiongozi mpya,
Balozi John William Kijazi amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumuamini na
kumteua pia amesema anaelewa majukumu ya katibu mkuu kiongozi katika Serikali ikiwemo kusimamia mazingira ya Watumishi, nidhamu kwa watumishi
pamoja na kuwa kiungo kikuu katika kumuunganisha Rais na wizara zake
halikadhalika kumshauri Rais katika Masuala ya utumishi.
“Natarajia kufanya kazi kwa
karibu na watendaji wote wa wizara zote wakiwemo Mawaziri,makatibu
wakuu na watendaji wengine ili kujua yale yanatokea kwenye wizara zao
na kujua yatakayohitaji maamuzi au ushauri katika maamuzi ya mkutano wa
Baraza la Mawaziri na Maadhimio yake nitayafuatilia kwa kila waziri
kwenye eneo kuhakikisha anatekeleza Maadhimio Hayo,”alisema Balozi
Kijazi.
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi Mpya
aliendelea kusema anaelewa kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria
kusimamia ukusanyaji wa Mapato pamoja na kupambana na rushwa hivyo Amejipanga kusimamia yote hayo na kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa
wa kutukuka na Wenye tija kwa kuzingatia nidhamu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
Kiongozi aliyemaliza muda wake, Balozi Ombeni Sefue amesema Anamshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli kwani haikuwa na lazima yeye kuendelea naye lakini aliweza
kumpa muda wa kufanya kazi nae. Pia alisema anamtakia Katibu Mkuu
Kiongozi mpya kila la heri katika utendaji na Atakuwa tayari kumpa
ushirikiano kila atakapohitaji.
Hata hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi
mpya alisema msamiati wa kutumbua majipu maana yake ni kutafuta Nidhamu
ndani ya Serikali na pale ambapo pana kasoro kurekebisha hivyo nae Atamsaidia Mheshimiwa Rais hilo ili kuleta mafanikio katika taifa kama
serikali ya awamu ya Tano ilivyodhamiria na kauli mbiu ya HAPAKAZI TU.
Balozi Ombeni Sefue aliteuliwa na
Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete na Baadae kuteuliwa na kufanya kazi na Mheshimiwa Dkt.John Pombe
Magufuli katika Serikali yake ya awamu ya Tano kwenye kipindi cha Mpito.
No comments:
Post a Comment