Thursday, 3 March 2016

Tuunge mkono haki sawa na ushiriki wa wanawake katika maendeleo.

02
Na Tabu Mullah
Watanzania na wadau wa Haki za wanawake nchini Wameshauriwa kuunga Mkono Haki sawa na Ushiriki kwa wanawake katika fursa za Uongozi wa kisiasa na kiuchumi na kupima Mafanikio Yaliyofikiwa na kuweka Mipango yenye Matokeo Makubwa. 
Akitoa Taarifa Juu ya Siku ya wanawake Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Wanawake Bi Sihaba Nkinga amesema kuwa Siku ya Wanawake Duniani Husisitiza kujenga Mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha Jamii kutafakari kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku  hiyo ya kila Mwaka.
Amesisitiza kuwa Wananchi Wametakiwa  pia  kubainisha Shuhuda za wanawake Waliotoa Mchango Uliotukuka katika kuwezesha Maendeleo ya Wanawake na Taifa kwa Ujumla na Tafakuri Hii Hufanywa kwa kuelimisha jamii kuhusu Jitihada Mbalimbali zilizofanywa na Serikali Na Asasi Mbalimbali yakiwemo Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake Na kuhamasisha Jamii kuhusu utekelezaji wa sera na Mipango Mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo kwa Wanawake kwa Ujumla.
“Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha Uamuzi kuwa, Maadhimisho Haya yafanyike Kitaifa kila Baada ya Miaka Mitano ili kutoa Muda wa Utekelezaji wa Maazimio na kupima Mafanikio Yaliyofikiwa katika kipindi cha Miaka Mitano”Alisema Bi Sihaba.
Sihaba Nkinga amewashauri Wanahabari Wote kuelimisha Jamii kuhusu kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake kwa Mwaka 2016 inayosema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”, ambapo Kauli Mbiu hii inasisitiza kuwa na Mikakati Thabiti yenye Mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 Yenye Malengo ya kufikia asilimia 50 kwa 50 ya Ushiriki wa Wanawake na Wasichana katika Nyanja zote za Maendeleo.
Aidha Bi Sihaba Nkinga Amemtaka kila Mtanzania aweze kutambua Jukumu alilonalo katika kufikia lengo la Ushiriki Sawa wa Wanawake na wasichana katika Uchumi; Afya, Elimu, Ajira, Sheria na Siasa ifikapo Mwaka 2030.
Kwa mwaka  2016, katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani,mikoa yote Nchini itazingatia Hali na Mazingira ya Mikoa husika na kwa  Mkoa wa Dar es Salaam Siku hii itaadhimishwa  katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa Mikoa yote kuhamasisha Wananchi na Wadau Wote kushiriki Maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia Ujumbe wa kauli Mbiu ya Mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment