Meneja
wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan
Mshakangoto akitoa Ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari kuhusu Taratibu Zinazotakiwa kuzingatiwa Na Taasisi za Serikali katika kuimarisha Matumizi Sahihi na Salama ya Teknolojia ya Habari Na Mawasiliano katika
kuendesha Mifumo ya Tehama Serikalini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimizi
wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba akifafanua
kuhusu mpango wa Serikali wa kuimarisha mawasiliano katika mifumo ya TEHAMA Serikalini.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
Na Chrispino Mpinge
Wakala
ya Serikali mtandao (e-Government Agency) imezishauri Taasisi zote Za
Umma ,Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekreterieti za Mikoa, Wakala na
Mamlaka za Serikali ,Bodi, Tume, Mabaraza, Mifuko, Mashirika ya umma na
Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata miongozo na viwango vilivyotolewa
Wakala hiyo katika uanzishaji na usimamizi wa mifumo ya
Tehama Serikalini.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan Mshakangoto Alipokuwa akitoa maelekezo na ufafanuzi wa taratibu
zinazotakiwa kuzingatiwa na taasisi hizo kwa lengo la kuimarisha
matumizi sahihi na salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika
kuendesha mifumo ya Tehama Serikalini.
Bi.
Mshakangoto amesema kuwa miongozo na viwango hivyo vinalenga
kuziwezesha taasisi za umma kujenga mifumo inayoendana na mahitaji
halisi ya Taasisi husika na kuepuka mifumo inayojengwa kwa shinikizo la
wafanyabiashara, wafadhili au kwa matakwa ya mtu binafsi.
“
Taasisi zote zikitumia miongozo ya viwango tuliyoweka, Serikali itakuwa
na uwezo wa kuepuka urudufu wa mifumo na kupunguza gharama kubwa za
uendeshaji kwa kuwa na mifumo endelevu yenye gharama halisi inayofuata
viwango vya Usalama katika kulinda taarifa na data za Serikali” Alifafanua Meneja huyo.
Amezishauri
taasisi hizo kuwasilisha maandiko ya mifumo mipya ya TEHAMA na kujaza
taarifa za mifumo au miradi ya TEHAMA iliyopo katika mfumo wa kukusanya
na kutunza taarifa za miradi ya TEHAMA Serikali ili iweze kuthibitishwa
iwapo imefuata miongozo na viwango vilivyowekwa kabla ya kujengwa na
kusakinishwa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au Utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini amesema kuwa wanashauriwa
kufuata miongozo na viwango hivi ili kujua mahitaji halisi ya Serikali
na kuweza kujenga mifumo ya TEHAMA endelevu na inayoleta tija kwa umma.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Usimizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari Na
Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba ameeleza kuwa mpango wa
Serikali ni kuhakikisha kuwa mifumo yote ya TEHAMA ya Serikali inakuwa
na mawasiliano na kubadilishana taarifa mbalimbali.
Amesema
kuwa Serikali imekuwa ikiweka msisitizo wa matumizi ya TEHAMA kwa lengo
la kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuwawezesha wananchi Na wadau
mbalimbali kupata huduma za Serikali kwa gharama nafuu kwa njia ya
Mtandao.
Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2012
kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala hii ina majukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.
kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala hii ina majukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment