Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo Tanzania (BMT) Bi. Zaynab Matitu akiongea na waandishi wa Habari
hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5
mwaka huu ili kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani katika uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa wa Baraza hilo Bw.
Diomiz Malinzi.
Mwenyekiti wa wa Baraza la
Michezo Tanzania (BMT) Bw. Diomiz Malinzi akiongea na waandishi wa
Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi
5 mwaka huu ili kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani katika uwanja
wa Uhuru jijini Dar es salaam kulia ni Makamu Mwenyekiti Bi. Zaynab
Matitu.
DK. AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOKWEPA KULIPA KODI
Na Chrispino Mpinge
WAZIRI wa Fedha na Mipango ,
Dakta Philipo Mpango, amesisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa
kodi zao kwa wakati na kuwaonya wale wote ambao watakwepa
watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria ili kuboresha huduma za jamii na
maendeleo ya taifa.
Alisema kuwa serikali mkakati
wa serikali ni ni kuongeza makusanyo na kulinda utulivu wa uchumi
ukuaji wake kwa kasi zaidi kwa kuwa wafanyabiashara ndio injini ya
chumi wa taifa.
Alisema nchi yetu ina utajiri
mkubwa wa raslimali ila bado nchi ni masikini akasisitiza umuhimu wa
kila mmoja kulipa kodi na kuwahakikishia kuwa serikali haitamuonea
mfanyabiashara yeyoyte na badala yake kutajengwa mazingira ya
kuwawezesha kulipa kodi bila usumbufu.
Ametumia fursa hiyo kuwaonya
wafanyabiashara ambao wanashirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka
ya mapato TRA, ambao sio waadilifu kukwepa kodi watatumbuliwa majipu
Alisema serikali itanunua
mashine za EFD na kuzigawa kwa wafanyabiashara wote bure lengo ni
kuhakikishia zinatumika katika manunuzi na mauzo ya bidhaa kwa ajili ya
kutolea risti kwa mununuzi.
Amesema lengo la kuhakikisha
kila mmoja anatimiza wajibu wa kulipa kodi ili kujenga Tanzania mpya
yenye uchumi wa viwanda,na hiyo ndio vipaumbele vya mwaka wa fedha
2016/17.
Alisema atafuta kodi zote
ambazo ni kero na tayari wizara imeshaziandikia wizara zingine na
halmashauri kuainisha kodi zenye kero ili zifutwe kwenye bajeti ijayo.
Wakichangia kwenye kikao hicho
wafanyabiashara wameihakikishia serikali kuwa watalipa kodi ila wanataka
kushirikishwa kwenye utungaji wa sera .
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha,
Felix Ntibenda,amesema mkoa wa Arusha unakumbana na changamoto
mbalimbali zikiwemo za sekta ya madini kuwa na makusanyo kidobo
kutokana na madini kutoroshwa kwa kupitia mpakani kutokana na eneo la
mpaka kuwa kubwa mno.
Waziri alikuwa akizungumza na
wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha ili kuwasikiliza kero zao ambazo
zinasababisha kodi kutokulipwa ipasavyo na hivyo kuikosesha serikali
mapato.
Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi Tamasha la Wanawake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark
Bi. Agnes Mgongo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu
tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia
litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kushoto kwake ni Mratibu wa tamasha hilo Bi. Anawery Phares
na kulia ni mshehereshaji (MC Pilipili) Bw. Emanuel Mathias.
Mratibu wa Tamasha la pamoja la
kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016
Bi. Anawery Phares(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Bi. Samia Suluhu Hassan,Kushoto ni Mwanamuzi wa Taarabu Bi. Patricia
Hillary na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi.Agnes Mgongo.
Mchekeshaji na Mshehereshaji Bw.
Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili akito kionjo cha mojawapo ya
kichekesho atakachokifanya siku ya tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku
ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016,kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo na kulia ni Mwakilishi wa
Children Survial Hut Tanzania (CSI) Bi.Stella Mranda.
Msanii wa Muziki wa Taarabu
Nchini Bi .Patricia Hillary akieleza jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kwa tamasha la
pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5
Machi, 2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Na Kalonga Kasati
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia
litakalofanyika Machi 5, 2016.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo ambalo litafanyika
katika ukumbi wa King Solomoni uliopo Nanga jijini Dar es salaam kwa
kujumuisha jinsia zote .
Ameongeza kuwa Kampuni ya Trumark
imeandaa tamasha hilo kwa lengo la kuwahamasisha Wanawake kuwa na nguvu
katika nafasi ya kuchangia na kuinua uchumi na maendeleo ya nchini.
“Ni kweli wapo wanawake wenye
mafanikio lakini kuna changamoto zinawakabili ikiwemo Uchache wa
ushiriki wa wanaume katika kufanikisha mafanikio ya wanawake na kufungua
fursa ili waweze kuwa sehemu ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali za
kiuchumi na kijamii” alifafanua Agnes.
Mbali na hayo Bi. Agnes amesema
kuwa kila mtu kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu Ya Maendeleo,
hivyo kila mtu na mahali popote alipo ashiriki vyema kutimiza wajibu
wake huku wakishirikiana na kusaidiana kwa pamoja ili kujenga taifa.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka
shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya Watoto na
wanawake (CSI Tanzania) nchini Stelala Mranda amesema kuwa wameahidi
kuwawezesha wanawake 20 watakaotaka kuhudhuria tamasha hilo.
Wadau mbalimbali wakiwemo Marie
stopes Tanzania, CSI Tanzania, wamejitokeza kudhamini tamasha hilo
lililobeba kauli mbiu isemayo “Pamoja tutafanikisha”.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza
saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa Njia za
uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki
na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza
saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa Njia za Uzazi wa Mpango, Upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki
na wananchi wote Watakao hudhuria tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment