Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionyeshwa eneo la uwanja wa ndege
itakakopita barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na
inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua eneo ambalo barabara ya
Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia
Utofu, Majani Mapana hadi Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads
Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads
Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo katika makutano ya
barabara ya mchepuko eneo la Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya gati ya Bandari ya
pangani ambayo inajengwa kwa gharama ya sh. bilioni 2.3.
Muonekano wa gati inayojengwa katika bandari ya Pangani iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya daraja la Mto
Pangani ambalo upembuzi yakinifu wa ujenzi wake umekamilika na litaanza
kujengwa hivi karibuni.
Na Fatma Rajabu
SERIKALI ipo kwenye hatua za
mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani ,Saadani mpaka
Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa kiwango cha lami ambapo mpaka
sasa tayari kazi iliyobaki ni kupata mzabuni wa kuendesha mradi huo.
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na
Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa ujenzi wa Barabara hiyo
utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 na
kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya
Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.
Mradi huo utaenda sambamba na
ujenzi wa Daraja katika Mto Pangani lenye urefu wa mita 550 ambalo
linategemewa kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya kuimarisha shughuli za
utalii katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa Prof.Mbarawa ni
kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo serikali itawalipa fidia
wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa tathimini kwa mujibu wa
sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.
“Nasisitiza kwamba kama sheria
inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai kila mwenye haki na
anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili hatalipwa na hii itakuwa
ni kulingana na tathmini iliyokwishafanyika……”,alisema Waziri huyo.
Alisema kuwa serikali inatambua
umuhimu wa ujenzi wa Barabara hiyo kwamba ndiyo kiini na moyo wa uchumi
wa wilaya ya Pangani hasa kwa kutambua namna ambavyo ina vivutio vingi
vya kitalii hatua itakayolenga kuwaongezea fursa za kibiashara wananchi
na kukuza Pato lao.
“Daraja hili litakuwa na uwezo wa
kupitisha magari na watembea kwa miguu kwa wakati mmoja na hivyo ni
mkombozi wa wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa walikuwa wakitegemea
kuvuka ng’ambo ya pili ya mto kwa kutumia kivuko tu ambacho wakati
mwingine kinakumbwa na hitilafu”,alifafanua Prof.Mbarawa ambaye yupo
mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.
Akizungumza wakati wa majumuisho
ya ziara yake baada ya kukagua Kivuko cha Mto Pangani,Barabara ya
Tanga,Saadani mpaka Bagamoyo na eneo linalotakiwa kujengwa
Daraja,Prof.Mbarawa aliuagiza Uongozi wa Wakala wa ufundi na
Umeme(Temesa)kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za utendaji wa kivuko kwa
kila siku.
Aliwaagiza kutumia mfumo wa
malipo kwa njia ya elektroniki ili kuepusha vitendo vya ubadhirifu wa
fedha wakati serikali ikiwa kwenye mpango wa ukusanyaji wa fedha kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Suala la kutumia mashine za
kieletroniki halina mjadala habari ya kutumia vitabu vya risiti ili Muongeze sifuri mbele hatuzitaki….hapa kuna shida kuna siku I naandikwa
imeingia shilingi Milioni moja lakini Benki zimeenda laki nane na
hamsini hii laki moja na hamsini zinaishia wapi hili ni tatizo”,alisema.
Hata hivyo alisema ipo haja kwa
Temesa kuajiri manahodha wa vivuko ambao wanafanya kazi kwa viwango vya
kitaaluma ambavyo vinakubalika badala ya kutumia Wazee ambao wanafanya
kazi kwa mazoea.
No comments:
Post a Comment