Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete Mh.Noramn Sigalla wakati
alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni moja ya Mashamba makubwa
ya kufuga Ng’ombe wa kisasa aina ya Mitamba.
Huwa
ni mfano wa Ng’ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la
kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara
moja kwa kila mmoja.
Mwigulu
Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo
kuhusiana na uzalishaji wa Ng’ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya . Makete Ndg
Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye
shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali yanayohusiana na kuyumba kwa
ufugaji wa ng’ombe kwenye shamba hilo.
Moja ya Farasi ambaye anafugwa
kwenye shamba la Kitulo,Idadi ya Farasi wanaofugwa imepungua kutokana na
wengi kuuzwa kwa wananchi.
Moja ya Dume la Ng’ombe la kisasa ambalo limezalishwa Shamba la kitulo.
Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia namna ukamuaji wa maziwa unavyofanyika kwenye shamba la kitulo.
Akiwa njiani kutokea shamba la
Kitulo,Mh.Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa
kata ya kikondo ambao walikuwa na malalamiko ya kulipwa fidia baada ya
kuhamishwa kutoka hifadhi ya Kitulo,Madai yao ya fidia ni fedha ya
Tanzania Bilion 1.8,Mwigulu amewaahidi kuwasaidia wananchi hao kwa
kuzungumza na waziri wa Mali asili na Utalii aweze kuprocess malipo
hayo.
Mbunge wa Makete,Dr.Norman
Sigalla akiomba kwa Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi kufanikisha zoezi
la kuboresha shamba la kitulo ili uchumi wa wananchi wake wa Makete na
wanaozunguka shamba hilo uimarike.
Na Divine Kweka
Shamba la Kitulo la Ufugaji wa
Ng’ombe aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo
la kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng’ombe aina ya Mitamba
wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na
nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya
kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza
kuwa 19 Centgrade.
Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la
kitulo ambalo linauwezo wa kulisha ng’ombe elfu nne (4000),Shamba hilo
kwa sasa lina ng”ombe mia saba tu(700).
Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia
ndama na kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa
kwaajili ya malisho haulidhishi.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto
zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng’ombe,Ameahidi
kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng’ombe wa
kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata
kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment