Na Tabu Mullah
Wanawake nchini wamehimizwa
kushiriki kwenye michezo mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa
ili kuboresha afya zao na kujiongezea kipato.
Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
leo jijini Dar es Salaam wakati akihutubia kwenye Tamasha la Michezo kwa Wanawake lililoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuelekea
kilele cha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Akihutubia kwa niaba ya Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Jenista ameeleza kuwa Serikali
ina mipango thabiti ya kuboresha sekta ya michezo hivyo ni wakati
muafaka kwa Wanawake wa rika zote kushiriki kwenye michezo kwa manufaa
yao na taifa kwa ujumla.
“Wanawake tunaweza tusisubiri
kuwezeshwa tujitokeze kwenye michezo kuanzia kwenye maeneo tunayoishi
kwani itatusaidia kuimarisha afya zetu na kuepuka majanga ikiwemo UKIMWI
hasa kwa wasichana kwa kuwa wanaposhiriki kwenye michezo wanaepuka
kujihusisha na vitendo viovu kama ulevi na uasherati vinavyopelekea
maambukizi” alisema Mhe. Jenista.
Aidha Mhe. Jenista amelitaka
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuandaa program maalum za kuhamasisha
makundi mbalimbali kushiriki kwenye michezo hasa wanawake, watoto na
walemavu.
Pia Mhe. Jenista ametoa wito
kwa wadau wa michezo ikiwemo Mifuko ya Hifadhi za Jamii kushirikiana na
BMT kuandaa matamasha mengi ya michezo yatakayohusisha wanachama wa Mifuko hiyo ili kuimarisha afya zao na kuepuka maradhi kama Shinikizo la
Damu na Kisukari Yanayosababisha mifuko hiyo kutumia gharama kubwa
kuwatibia kupitia fao la matibabu.
Kwa upande wake Makamu
Mwenyekiti wa BMT Mhe. Zainab Vullu (Mb) ameiomba Serikali kutatua
changamoto zinazoikabili sekta ya michezo ikiwemo kupunguza kodi kwa
vifaa vya Michezo vinavyoingia nchini na kuboresha mitaala ya elimu ya
michezo mashuleni.
Tamasha hilo la michezo kwa
wanawake limefanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
likibeba kauli mbiu ya mwaka huu inayosema ” 50 kwa 50 ifikapo 2030,
Tuongeze Jitihada, Maendeleo ya Wanawake kupitia Michezo Inawezekana”.
MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI JUU YA MWELEKEO WA HALI YA MVUA NCHINI
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati) akitoa taarifa ya Mwelekeo
wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei,
2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja Kitengo Kikuu cha Habari
TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa ambae ni Mkurugenzi
Huduma za Utabiri TMA.
Mamla
ka ya Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na
Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji, kujiandaa juu ya namna ya
kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika
ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza,
wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.
wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.
Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili
ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika
maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika
maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
Alisema
Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika Maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali
ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi
zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia Taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
No comments:
Post a Comment