
Na Nechi Makundi
SERIKALI imefuta hati za
mashamba makubwa 13,ambayo kwa muda mrefu yamekuwa Hayaendelezwi na
kuyakabidhi kwa uongozi wa wilaya ya Monduli ili yagawiwe kwa wananchi
ambao hawana ardhi.
Shughuli hiyo ya kukabidhi
mashamba hayo imefanyika kwenye kata mbili za Lokisale na Olmot
,wilayani Monduli, kwenye mkutano wa hadhara .
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya
makazi Wiliam Lukuvi, amesema mashamba hayo yalikuwa Yakimilikiwa na
wawekezaji ambao hawayajaendeleza kwa kipindi kirefu yapo vijiji vya
Mswakini na Lokisale.
Aidha waziri Lukuvi ameuagiza
uongozi wa halmashauri ya Monduli, kumpatia orodha ya mashamba mengine
39,ambayo hayajaendelezwa kabla ya mwosho wa Marchi mwaka huu ili nayo
yafutiwe hati na kuyagawa kwa wananchi ambao hawana mashamba wilayani
humo.
Waziri Lukuvi, amesema kuwa
serikali inawahitaji wawekezaji wa kweli ambao watayaendeleza Maeneo
lakini sio ambao wameyatelekeza mashamba hguku wananchi wakikosa
mashamba ya kulima .
Waziri, Lukuvi,amesema
uwekezaji kwenye mashamba lazima uambatane na utoaji wa ajira za kudumu
na sio vibarua na ajira iwe ni chanzo muhimu na kusisitiza wawekezaji
ambao hawataki kutoa ajira warudishe ardhi hiyo waliyoimiliki.
Amewaambia kuwa ardhi ambayo
mwekezaji ameshindwa kuiendeleza ikifutiwa umiliki wake haitalipwa fidia
kwa kuwa mhusika ameshindwa kuiendeleza na ameitelekeza.
Waziri, amesisitiza kuwa
kipaumbele cha ardhi inayofutiwa hati miliki ni kwa wananchi maskini na Sio wenye uwezo, wenye ardhi au viongozi la hasha bali kipaumbele ni kwa
wale ambao hawana kabisa ardhi.
Aidha amezuia maafisa ardhi
ngazi za kanda nchini kutokujihusisha na uhamishaji wa umiliki wa Ardhi
na mashamba au kusajili mashamba mapya na kutoa hati miliki mpaka
waziri ataarifiwe kwanza.
Amesema amegundua kuna ujanja
ujanja, unaotumiwa na wamiliki wa mashamba ambao huyauza na kusajili
maeneo yaliyobakia jambo ambalo ni kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment