Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi Mhasibu
wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau
wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia
timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Fedha hizo zimewekwa
katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677
inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimsikiliza Mhasibu
wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni
tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe
kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars.
Ijumaa ya wiki hii timu hiyo itacheza na Zimbabwe mashindano ya
awali ya kufuzu kombe la Afrika kwa wanawake.
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimweleza jambo
Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi
shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka
jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa
miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha hizo katika
Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa
jina la Twiga Stars Special Fund”.
Serikali yalitaka Dira ya Mtanzania kukanusha tuhuma Dhidi ya Balozi Ombeni Sefue
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw.Assah Mwambene (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za
upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la tarehe
29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw.Jamal Zuberi na
Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw.Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya Habari
(MAELEZO).
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari, Bw.Assah Mwambane (ambaye hayupo katika picha) iliyokuwa
ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha habari waliyoitoa
hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue
Ikulu”.
Na Kalonga Kasati
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw.Assah Mwambene ameutaka uongozi wa Gazeti la Dira ya
Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa waliyoitoa katika
toleo namba 404 la tarehe 29/02/2016 lenye kichwa cha Habari “Uchafu
wa Ombeni Sefue Ikulu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na Waandishi Wa habari
kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala
kuhusika na kampuni ya CRJE katika utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu
cha Dodoma Oktoba 2007 kwani katika kipindi hicho alikuwa Balozi wa
Tanzania nchini Marekani.
“Serikali inautaka uongozi wa
Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo kwa uzito ule Uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga wakidai wana
ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwemo
Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema Bw.Mwambene.
Aidha, Bw.Mwambene amesema
gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
alipigia chapuo Kampuni ya “UGG” iliyowahi kuonyesha nia ya kujenga
reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya kweli na hakuna kampuni
yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya kujenga reli hiyo.
Mkurugenzi aliendelea kusema kuwa
gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati alichokifanya Balozi
Sefue ilikuwa ni kusoma Matokeo ya Uchunguzi ambao hakuufanya yeye.
Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji
wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi huo.
Hata hivyo serikali imewashauri Wamiliki wa vyombo vya habari,wachapishaji,wahariri, na Waandishi wa Habari wajikite kwenye weledi na ukweli pia wafanye Utafiti wa kina na
kuandika Mambo waliyo na uhakika nayo
No comments:
Post a Comment